Sehe mu B i Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Sehemu B ya Sheria ya Elimu ya Watu Walemavu (IDEA). Kumbuka: Marejeo yote ya wilaya ya shule yanatumika kwa chombo cha umma kinachowajibika. Faharasa Ilani Iliyoandikwa Mapema......................................................................................... 1 Lugha Asili ................................................................................................................. 2 Barua ya Elektroniki...................................................................................................2 Ruhusa ya Mzazi - Ufafanuzi ..................................................................................... 2 Ruhusa ya Mzazi ....................................................................................................... 3 Tathmini zenye Kujitegema za Kielimu ...................................................................... 5 Ufafanuzi.................................................................................................................... 6 Inayoweza Kutambuliwa na Mtu Binafsi..................................................................... 7 Ilani kwa WAzazi........................................................................................................ 7 Haki za Ufikiaji ........................................................................................................... 7 Rekodi ya Ufikiaji ....................................................................................................... 8 Rekodi za Zaidi ya Mtoto Mmoja................................................................................ 8 Orodha ya Aina na Maeneo ya Habari....................................................................... 8 Ada ............................................................................................................................ 8 Kurekebishwa kwa Rekodi Mzazi Akiomba................................................................ 9 Nafasi ya Kusikilizwa ................................................................................................. 9 Utaratibu wa Kusikilizwa ............................................................................................ 9 Matokeo ya Kusikilizwa..............................................................................................9 Ruhusa ya Kufichua Habari za Kibinafsi zinazoweza Kutambuliwa......................... 10 Kuhifadhi.................................................................................................................. 10 Uharibifu wa Habari ................................................................................................. 10 Utofauti kati ya Malalamiko ya Kusikilizwa kwa Mchakato Unaotazamiwa na Utaratibu wa Malalamiko ya Serikali........................................ 11 Kuchukuliwa kwa Utaratibu wa Malalamiko ya Serikali............................................ 11 Utaratibu wa Chini wa Malalamiko ya Serikali ......................................................... 12 Kuwasilisha Malalamiko........................................................................................... 13 Kuwasilisha Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa............................................. 14 Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa................................................................. 14 Fomu za Mfano........................................................................................................ 16 Upatanisho............................................................................................................... 16 Sehe mu B ii Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Mahali pa Mtoto Wakati Kusikilizwa na Malalamiko ya Mchakato Yakisubiri .............................................................................................................. 18 Mchakato wa Suluhisho ........................................................................................... 18 Kusikilizwa kwa Mchakato adilifu unaotazamiwa ..................................................... 20 Haki za Kusikilizwa .................................................................................................. 22 Maamuzi ya Kusikilizwa ........................................................................................... 22 Kukamilika kwa uamuzi; Kukata rufaa; Uhakiki adilifu ............................................. 23 muda maalum na Urahisi wa Kusikilizwa na Uhakiki ............................................... 23 Hatua za Madai, Pamoja na Kipindi cha Muda ambao Unaweza Kuwasilisha Hatua hizo ......................................................................................... 24 Ada ya Wakili ........................................................................................................... 25 mamlaka ya mtumishi wa shule ............................................................................... 26 Mabadiliko ya Mahali kwa Sababu ya Uhamisho wa Kinidhamu ............................. 29 Uamuzi wa Mpangilio............................................................................................... 29 Kukata rufaa ............................................................................................................ 30 Mahali Wakati wa Kukata rufaa ............................................................................... 31 Ulinzi kwa Watoto ambao Hawajastahiki Elimu Maalum na Huduma Zinazolingana........................................................................................................ 31 Rejeleo la hatua ya Watekeleza Sheria na Watawala wa kimahakama.................. 32 Kwa ujumla .............................................................................................................. 33 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 1 Habari kwa ujumla ILANI ILIYOANDIKWA MAPEMA 34 CFR §300.503 Ilani Wilaya ya shule yako ni lazima ikupe ilani iliyoandikwa (ikupe habari maalum kwa kuandika), wakati wowote inapo: 1. Pendekeza kuanzisha au kubadilisha kitambulisho, tathmini, au mahali pa elimu ya mtoto wako, au utoaji wa elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) kwa mtoto wako; au 2. Kataa kuanzisha au kubadilisha kitambulisho, tathmini, au mahali pa elimu ya mtoto wako, au utoaji wa FAPE kwa mtoto wako. Yaliyomo kwenye ilani Ilani iliyoandikwa ni lazima: 1. Ifafanue hatua ambayo wilaya ya shule yako inapendekeza au inayokataa kuchukua; 2. Ieleze ni kwanini wilaya ya shule yako inapendekeza au inakataa kuchukua hatua hiyo; 3. Ifafanue kila utaratibu wa tathmini, uchunguzi, rekodi, au ripoti ambayo wilaya ya shule yako ilitumia katika kuamua kupendekeza au kukataa hatua hiyo; 4. Ijumuishe taarifa ya kwamba una ulinzi chini ya utoaji wa kuhifadhi utaratibu katika Sehemu B ya IDEA; 5. Ikuambie vile unavyoweza kupata ufafanuzi wa kuhifadhi utaratibu kama hatua ambayo wilaya ya shule yako inapendekeza au inakataa sio rejeleo halisi la tathmini; 6. Ijumuishe rasilimali unazoweza kurejelea ili kukusaidia kuelewa Sehemu B ya IDEA; 7. Ifafanue chaguzi zingine ambazo Kikundi cha mpango wa elimu ya kibinafsi ya mtoto wako (IEP) ilionelea na sababu ambazo chaguzi hizo zilikataliwa; na 8. Itoe ufafanuzi wa sababu zingine za kwanini wilaya ya shule yako ilipendekeza au ilikataa hatua hiyo. Ilani katika lugha inayoeleweka Ilani lazima iwe: 1. Imeandikwa katika lugha inayoeleweka na umma kwa ujumla; na 2. Imetolewa katika lugha yako ya asili au hali nyingine ya kuwasiliana unayotumia, isipokuwa kama haiwezi kufanyika hivyo waziwazi. Ikiwa lugha yako ya asili au hali nyingine ya kuwasiliana sio lugha iliyoandikwa, wilaya ya shule yako ni lazima ihakikishe kwamba: 1. Ilani hiyo imetafsiriwa kwa kusema kwa hali zingine katika lugha yako ya asili au hali nyingine ya kuwasiliana; 2. Unaelewa yaliyomo kwenye ilani; na 3. Kuna ushahidi uliyoandikwa ya kwamba 1 na 2 walipatana. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu LUGHA ASILI 2 34 CFR §300.29 Lugha asili, inapotumiwa na mtu ambaye afahamu Kiingereza vizuri, inamaanisha yanayofuata: 1. Lugha ambayo kwa kawaida inatumiwa na mtu huyo, au, kwa hali ya mtoto, lugha ambayo kwa kawaida hutumiwa na wazazi wa mtoto; 2. Katika kuwasiliana moja kwa moja na mtoto (ikijumuisha tathmini ya mtoto), lugha ambayo kwa kawaida hutumiwa na mtoto nyumbani au katika mazingira ya kujifunza. Kwa mtu ambaye ni kiziwi au kipofu, au mtu ambaye hana lugha iliyoandikwa, hali ya mawasiliano ni ile mtu huyo kwa kawaida hutumia (kama vile lugha ya ishara, au mawasiliano ya kusema). BARUA YA ELEKTRONIKI 34 CFR §300.505 Ikiwa wilaya ya shule yako inawapa wazazi chaguo la kupokea hati kwa barua pepe, unaweza kuchagua kupokea yafuatayo kwa barua pepe: 1. Ilani iliyoandikwa mapema; 2. Ilani ya kuhifadhi utaratibu; na 3. Ilani zinazohusiana na malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. RUHUSA YA MZAZI -UFAFANUZI 34 CFR §300.9 Ruhusa Ruhusa inamaanisha: 1. Umejulishwa vikamilifu katika lugha yako ya asili au hali zingine za kuwasiliana (kama vile lugha ya ishara, Braili, au mawasiliano ya kusema) habari zote kuhusu hatua ambayo unapeana ruhusa. 2. Unaelewa na kukubali kwa kuandika hatua hiyo, na ruhusa hiyo inafafanua hatua hiyo na inaorodhesha rekodi (kama kuna yoyote) ambayo itatolewa na kwa nani; na 3. Unaelewa kwamba ruhusa hiyo ni ya kujitolea kwa sehemu yako na unaweza kuondoa ruhusa yako wakati wowote. Wewe kuondoa ruhusa haikanushi (kuondoa) hatua ambayo ilitekelezwa baada yako kupeana ruhusa na kabla ya wewe kuiondoa. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu RUHUSA YA MZAZI 3 34 CFR §300.300 Ruhusa ya tathmini ya kwanza Wilaya ya shule yako haiwezi kutekeleza tathmini ya kwanza ya mtoto wako ili kuamua kama mtoto wako anastahiki chini ya Sehemu B ya IDEA kupokea elimu maalum na huduma zinazohusiana bila ya kwanza kukupa ilani iliyoandikwa mapema ya hatua iliyopendekezwa na bila ya kupata ruhusa yako kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Ruhusa ya Mzazi. Wilaya ya shule yako ni lazima itie bidii ili kupata ruhusa yako unayoifahamu kwa ajili ya tathmini ya kwanza ili kuamua kama mtoto wako ni mtoto ambaye ana ulemavu. Ruhusa yako ya tathmini ya kwanza haimaanishi kwamba umepeana pia ruhusa yako kwa wilaya ya shule kuanza kupeana elimu maalum na huduma zinazohusiana kwa mtoto wako. Ikiwa mtoto wako ameandikishwa katika shule ya umma au unatafuta kumwandikisha mtoto wako katika shule ya umma na umekataaa kupeana ruhusa au umeshindwa kujibu ombi la kupeana ruhusa ya tathmini ya kwanza, wilaya ya mtoto wako inaweza, lakini haipaswi, kutafuta kutekeleza tathmini ya kwanza ya mtoto wako kwa kutumia Sheria ya upatanisho au malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, mkutano wa suluhisho, na utaratibu wa kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa (isipokuwa ikitakikana kufanywa hivyo au imekatazwa kufanywa hivyo chini ya sheria za Serikali). Wilaya ya shule yako haitakeuka uwajibikaji wake wa kumpata, kumtambua na kumtathmini mtoto wako kama haitafuata tathmini ya mtoto wako katika hali hizi, isipokuwa sheria za Serikali zinahitaji ifuate tathmini hio. Sheria maalum za tathmini ya kwanza ya wanaolindwa na Serikali Ikiwa mtoto analindwa na Serikali na haishi na wazazi wake — Wilaya ya shule haitaji ruhusa ya tathmini ya kwanza kutoka kwa mzazi ili kuamua kama mtoto huyo ni mtoto mlemavu kama: 1. Licha ya jitihada za kufanya hivyo, wilaya ya shule haiwezi kumpata mzazi wa mtoto; 2. Haki za wazazi zimeondolewa kulingana na sheria za Serikali; au 3. Hakimu amepeana haki ya kufanya maamuzi ya kielimu na ruhusa ya tathmini ya kwanza kwa mtu ambaye si mzazi wa mtoto huyo. Anayelindwa na Serikali, kama inavyotumiwa katika IDEA, inamaanisha mtoto ambaye, kama ilivyoamuliwa na Serikali ambayo mtoto huo anaishi, ni: 1. Mtoto wa kulea; 2. Anayeonekana analindwa na Serikali chini ya sheria za Serikali; au 3. Aliye katika ulinzi wa chombo cha umma cha maslahi ya watoto. Anayelindwa na Serikali haimjumuishi mtoto wa kulea ambaye ana mzazi wa kumlea. Ruhusa ya mzazi ya huduma Wilaya ya shule yako ni lazima ipate ruhusa yako unayoifahamu kabla ya kupeana elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mtoto wako kwa mara ya kwanza. Wilaya ya shule yako ni lazima ijitahidi ili ipate ruhusa yako unayoifahamu kabla ya kupeana elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mtoto wako kwa mara ya kwanza. Usipojibu ombi la kupeana ruhusa yako kwa mtoto wako ili apokee elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mara ya kwanza, au ukikataa kupeana ruhusa kama hiyo, wilaya ya shule 4 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu yako haitatumia kuhifadhi utaratibu (k.m upatanisho, malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, mkutano wa suluhisho, au utaratibu wa kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa) ndiposa kupata makubaliano au uamuzi wa kuwa elimu hiyo maalum na huduma zinazohusiana (inayopendekezwa na Kikundi cha IEP cha mtoto wako) itapewa mtoto wako bila ya ruhusa yako. Ukikataa kupeana ruhusa yako kwa mtoto wako kupokea elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mara ya kwanza, au usipojibu ombi la kupeana ruhusa kama hiyo na wilaya ya shule haimpatii mtoto wako elimu maalum na huduma zinazolingana ambayo ilitafuta ruhusa yako kwa ajili yake, wilaya ya shule yako: 1. Haitakuwa imekeuka mahitaji ya kupeana elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) kwa mtoto kwa kukosa kwake kupeana huduma hizo kwa mtoto wako; na 2. Haihitajiki kuwa na mkutano wa mpango wa elimu ya kibinafsi (IEP) au kuanzisha IEP ya mtoto wako ya elimu maalum na huduma zinazolingana ambayo ruhusa iliombwa kwa ajili yake. Ruhusa ya mzazi ya kutathminiwa tena Wilaya ya shule yako ni lazima ipate ruhusa yako unayoifahamu kabla ya kutathmini tena mtoto wako, isipokuwa wilaya ya mtoto wako inaweza kuonyesha kwamba: 1. Ilichukua hatua zinazofaa za kupata ruhusa yako ya kutathmini mtoto wako tena; na 2. Haukujibu. Ukikataa kukubali mtoto wako atathminiwe tena, wilaya ya shule inaweza, lakini haitakikani, kufuatilia kutathminiwa tena kwa mtoto wako kwa kutumia upatanisho, malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, mkutano wa suluhisho, na utaratibu wa kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa ili itafute kubadili kukataa kwako kupeana ruhusa ya mtoto wako kutathminiwa tena. Sawasawa na tathmini za kwanza, wilaya ya shule yako haitakuwa imekeuka uwajibikaji wake chini ya Sehemu B ya IDEA ikikataa kufuatilia tathmini tena katika njia hii. Hati ya jitihada zinazofaa za kupata ruhusa ya mzazi Shule yako ni lazima itunze hati za jitihada zinazofaa za kupata ruhusa ya mzazi ya tathmini za kwanza, za kupeana elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mara ya kwanza, za kutathmini tena na kuwapata wazazi wa wanaolindwa na Serikali kwa tathmini za kwanza. Hati hiyo lazima iwe na rekodi ya majaribio ya wilaya ya shule katika maeneo haya, kama vile: 1. Rekodi za kina za simu zilizopigwa au zilizojaribiwa kupigwa na matokeo ya simu hizo; 2. Nakala za mawasiliano zilizotumiwa wazazi na majibu yoyote yaliyopokewa; na 3. Rekodi za kina za ziara zilizofanywa kwa nyumba ya mzazi au mahali pa ajira na matokeo ya ziara hizo. Mahitaji mengine ya ruhusa Ruhusa yako haihitajiki kabla ya wilaya ya shule yako: 1. Kuhakiki data zilizomo kama sehemu ya tathmini ya mtoto wako au kutathmini tena; au 2. Kumpatia mtoto wako mtihani au tathmini nyingine ambayo inapewa watoto wote isipokuwa, kabla ya mtihani huo au tathmini, ruhusa inahitajika kutoka kwa wazazi wote wa watoto wote. Wilaya ya shule yako haitatumia kukataa kwako kupeana ruhusa kwa huduma moja au shughuli ili kukunyima wewe au mtoto wako huduma zingine, manufaa, au shughuli. 5 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Ikiwa umemwandikisha mtoto wako katika shule ya kibinafsi kwa gharama yako mwenyewe au ikiwa unamfunza mtoto wako nyumbani, na haupeani ruhusa yako ya tathmini ya kwanza ya mtoto wako au mtoto wako kutathminiwa tena, au ulishindwa kujibu ombi la kupeana ruhusa yako, wilaya ya shule haiwezi kutumia utaratibu wake wa kubadili ruhusa (k.v., upatanisho au malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, mkutano wa suluhisho, na utaratibu wa kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa) na haihitajiki ili kumzingatia mtoto wako kama anayestahiki kupokea huduma za haki ( huduma zinazopatikana kwa watoto walemavu wa shule ya kibinafsi waliyowekwa hapo na wazazi). TATHMINI ZENYE KUJITEGEMA ZA KIELIMU 34 CFR §300.502 Kwa ujumla Kama ilivyofafanuliwa hapo chini, una haki ya kupata tathmini yenye kujitegemea ya kielimu (IEE) kwa mtoto wako ikiwa haukubaliani na tathmini ya mtoto wako ambayo ilipatikana na wilaya ya shule yako. Ukiomba tathmini yenye kujitegemea ya kielimu, wilaya ya shule ni lazima ikupe habari kuhusu ni wapi unaweza kupata tathmini yenye kujitegemea ya kielimu na kuhusu kanuni za wilaya ya shule ambayo hutumika kwa tathmini zenye kujitegemea za kielimu. Ufafanuzi Tathmini yenye kujitegemea ya kielimu inamaanisha tathmini inayotekelezwa na mtahini anayestahiki ambaye hajaajiriwa na wilaya ya shule ambayo inauwajibikaji wa elimu ya mtoto wako. Gharama ya umma inamaana kwamba wilaya ya shule italipa gharama yote ya tathmini au itahakikisha kwamba tathmini imetolewa bila malipo, kulingana na utoaji wa Sehemu B ya IDEA, ambayo uruhusu kila Serikali kutumia rasilimali yoyote ya Serikali, mitaa, Jimbo na kibinafsi ya usaidizi inayopatikana katika Serikali ili kufikia mahitaji ya Sheria ya Sehemu ya B. Haki ya mzazi ya tathmini kwa gharama ya umma Una haki ya tathmini yenye kujigemea ya kielimu kwa mtoto wako kwa gharama ya umma ikiwa haukubaliani na tathmini ya mtoto wako ambayo ilipatikana na wilaya ya shule yako, chini ya masharti yanayofuata: 1. Ukiomba tathmini yenye kujitegemea ya kielimu kwa mtoto wako kwa gharama ya umma, wilaya ya shule yako lazima, bila kupoteza muda wowote, aidha: (a) Iwasilishe malalamiko ya mchakato unaotazamiwa ili kuomba kusikilizwa ili ionyeshe kwamba mtoto wako anafaa; au (b) Itoe tathmini yenye kujitegemea ya kielimu kwa gharama ya umma, isipokuwa wilaya ya shule ionyeshe wakati wa kusikilizwa kwamba tathmini ya mtoto wako ambao ulipata haukufikia kanuni za wilaya ya shule. 2. Wilaya ya shule yako ikiomba kusikilizwa na uamuzi wa mwisho uwe kwamba tathmini ya mtoto wako ya wilaya ya shule yako inafaa, bado una haki ya tathmini yenye kujigemea ya kielimu, lakini sio kwa gharama ya umma. 3. Ukiomba tathmini yenye kijigemea ya kielimu kwa mtoto wako, wilaya ya shule inaweza kukuuliza ni kwanini unakataa tathmini ya mtoto wako iliyopatikana na wilaya ya shule yako. Walakini, wilaya ya shule yako haitahitaji ufafanuzi na haitapoteza wakati wa kutoa tathmini yenye kujigemea ya kielimu kwa mtoto wako kwa gharama ya umma au Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 6 kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa ili kuomba kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ili kulinda tathmini ya wilaya ya shule kwa mtoto wako. Una haki ya tathmini moja tu yenye kujigemea ya kielimu kwa mtoto wako kwa gharama ya umma kila wakati wilaya ya shule yako inapotekeleza tathmini ya mtoto wako ambayo haukubaliani nao. Tathmini zilizoanzishwa na mzazi Ukipata tathmini yenye kujitegemea ya kibinafsi kwa mtoto wako kwa gharama ya umma au unaoshiriki pamoja na wilaya ya shule tathmini ya mtoto wako ambayo ulipata kwa gharama za kibinafsi: 1. Wilaya ya shule yako lazima izingatie matokeo ya tathmini ya mtoto wako, kama inafikia kanuni za wilaya ya shule ya tathmini zenye kujitegemea za kielimu, katika uamuzi wowote uliofanywa kulingana na utoaji wa elimu ya bure ya umma inayotakikana (FAPE) kwa mtoto wako; na 2. Wewe au wilaya ya shule yako inaweza kuleta tathmini hiyo kama ushahidi wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa kuhusu mtoto wako. Maombi ya tathmini na maafisa wa kusikiza Kama afisa wa kusikiza akiomba tathmini yenye kujitegemea ya kielimu kwa mtoto wako kama sehemu ya kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa, gharama ya tathmini ni lazima igharamiwe na umma. Kanuni za wilaya ya shule Ikiwa tathmini zenye kujitegemea ya kielimu ni kwa gharama ya umma, kanuni ambayo tathmini hiyo inapatikana, pamoja na eneo la tathmini na sifa zinazostahili za mtahini, lazima ziwe sawa na kanuni ambayo wilaya ya shule hutumia inapoanzisha tathmini (hadi kanuni hizo zilingane na haki yako ya tathmini yenye kujitegemea ya kielimu). Isipokuwa kwa kanuni iliyofafanuliwa hapo juu, wilaya ya shule haiwezi kuweka masharti au muda maalum unaohusiana na kupata tathmini yenye kujitegemea ya kielimu kwa gharama ya umma. Siri za Habari UFAFANUZI 34 CFR §300.611 Kama ilivyotumiwa chini ya kichwa cha Siri za Habari: . Uharibifu unamaanisha uharibifu wa kimwili au kuondolewa kwa vitambulisho vya kibinafsi kutoka kwa habari ili habari hizo zisiweze kutambuliwa kibinafsi tena. . Rekodi za elimu inamaanisha aina za rekodi zilizoshughulikiwa chini ya ufafanuzi wa “rekodi za elimu” katika 34 CFR sehemu ya 99 (maagizo yanayotekeleza Sheria ya Siri na Haki ya Elimu ya Jamii ya mwaka wa 1974, 20 U.S.C. 1232g (FERPA). 7 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu . Chombo husika inamaanisha wilaya yoyote ya shule, chombo au taasisi ambayo ukusanya, kutunza, au kutumia habari za mtu binafsi zinazoweza kutambuliwa, au kutoka kule habari zinapatikana, chini ya Sehemu B ya IDEA. INAYOWEZA KUTAMBULIWA NA MTU BINAFSI 34 CFR §300.32 Inayoweza kutambuliwa na mtu binafsi inamaanisha habari ambazo zina: (a) Jina la mtoto wako, jina lako kama mzazi, au jina la mtu mwingine wa familia; (b) Anwani ya mtoto wako; (c) Kitambulisho cha kibinafsi, kama vile namba ya mtoto wako ya usalama wa jamii au namba ya mwanafunzi; au (d) Orodha ya tabia za kibinafsi au habari zingine ambazo zinawezesha kumtambua mtoto wako kwa uhakika. ILANI KWA WAZAZI 34 CFR §300.612 Chombo cha Serikali cha Elimu ni lazima kipeane ilani ambayo inatosha kuwajulisha vikamilifu wazazi kuhusu siri ya habari za mtu binafsi zinazoweza kutambuliwa, pamoja na: 1. Ufafanuzi wa kadiri ambayo ilani hiyo inapeanwa katika lugha za asili za vikundi kadhaa vya umma katika Serikali; 2. Ufafanuzi wa watoto ambao habari zao za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa zinatunzwa, aina ya habari zinazotafutwa, mbinu ambazo Serikali inakusudia kutumia ili kukusanya habari hizo (pamoja na vyanzo ambavyo habari ukusanywa), na matumizi yatakayofanyiwa habari hizo; 3. Muhtasari wa sera na utaratibu ambao vyombo husika lazima zifuate kuhusu kuhifadhi, kufichua kwa chama cha tatu, uzuiaji, uharibifu wa habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa; na 4. Ufafanuzi wa haki zote za wazazi na watoto kuhusiana na habari hizi, pamoja na haki chini ya Sheria ya Siri na Haki ya Elimu ya Jamii (FERPA) na maagizo yake yanayotekeleza katika 34 CFR Sehemu ya 99. Kabla ya shughuli yoyote kuu ya utambuaji, utafutaji, au tathmini (ijulikanayo pia kama "kumpata mtoto") ilani hiyo lazima ichapishwe au itangazwe kwenye gazeti au kwenye vyombo vingine vya habari, au zote, pamoja na mzunguko wa kutosha wa kuwajulisha wazazi katika Serikali yote juu ya shughuli ya kuwatafuta, kuwatambua, na kuwatathmini watoto wanaohitaji elimu maalum na huduma zinazolingana. HAKI ZA UFIKIAJI 34 CFR §300.613 Chombo husika ni lazima kikuruhusu kuchunguza na kuhakiki rekodi zozote za kielimu zinazohusiana na mtoto wako ambazo zilizokusanywa, zilizotunzwa, au zilizotumiwa na wilaya ya shule yako chini ya Sehemu B ya IDEA. Chombo husika ni lazima kifuate ombi lako la 8 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu kuchunguza na kuhakiki rekodi zozote za kielimu juu ya mtoto wako bila ya kupoteza wakati wowote na kabla ya mkutano wowote unaohusiana na mpango wa elimu ya kibinafsi (IEP), au kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa (pamoja na mkutano wa suluhisho au kusikilizwa kunakohusiana na tabia), na katika hali yoyote isiwe zaidi ya siku 45 za kalenda baada ya ombi lako. Haki yako ya kuchunguza na kuhakiki rekodi za kielimu inajumuisha: 1. Haki yako ya kujibiwa maombi yako ya maana juu ya ufafanuzi na utafsiri wa rekodi kutoka kwa chombo husika; 2. Haki yako ya kuomba kwamba chombo husika kitoe nakala za rekodi ikiwa hauwezi kuchunguza na kuhakiki vilivyo rekodi isipokuwa upokee nakala hizo; na 3. Haki yako ya mwakilishi wako kuchunguza na kuhakiki rekodi hizo. Chombo husika kinaweza kudhania kwamba unaidhini ya kuchunguza na kuhakiki rekodi zinazohusiana na mtoto wako isipokuwa washauriwe kwamba hauna idhini chini ya sheria za Serikali zinazotumika zinazosimamia masuala kama hayo ya ulezi, au kuachana na talaka. REKODI YA UFIKIAJI 34 CFR §300.614 Kila chombo husika ni lazima kitunze rekodi za vyama vinavyofikia rekodi za elimu zinazokusanywa, zinazotunzwa, au kutumiwa chini ya Sehemu B ya IDEA (isipokuwa wazazi na wafanyakazi walioidhinishwa wa chombo husika wanaofikia), pamoja na jina la chama, tarehe ambayo ufikiaji ulipeanwa, na kusudi la chama hicho kuidhinishwa kutumia rekodi hizo. REKODI ZA ZAIDI YA MTOTO MMOJA 34 CFR §300.615 Ikiwa rekodi yoyote ya elimu ina habari ya zaidi ya mtoto mmoja, wazazi wa watoto hao wana haki ya kuchunguza na kuhakiki habari zinazohusiana na watoto wao tu au kujulishwa habari hizo maalum. ORODHA YA AINA NA MAENEO YA HABARI 34 CFR §300.616 Ikiombwa, kila chombo husika ni lazima kikupe orodha ya aina na maeneo ya rekodi za kielimu zilizokusanywa, zilizotunzwa, au kutumiwa na chombo hicho. ADA 34 CFR §300.617 Kila chombo husika kinaweza kulipisha ada ya nakala za rekodi ambazo hukutengenezea chini ya Sehemu B ya IDEA, ikiwa ada hiyo haikuzuilii kutokana na kutekeleza haki yako ya kuchunguza na kuhakiki rekodi hizo. 9 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Chombo husika kinaweza kukosa kulipisha ada ya kutafuta au kuchukua habari chini ya Sehemu B ya IDEA. KUREKEBISHWA KWA REKODI MZAZI AKIOMBA 34 CFR §300.618 Ukiamini kwamba habari katika rekodi za elimu zilizokusanywa, kutunzwa, au kutumiwa kuhusu mtoto wako chini ya Sehemu B ya IDEA si sahihi, zinapotosha, au zinakeuka siri au haki zingine za mtoto wako, unaweza kuomba chombo husika ambacho kinatunza habari hizo kibadilishe habari hizo. Chombo husika ni lazima kiamue aidha kubadilisha habari hizo kulingana na ombi lako kati ya kipindi cha muda unaoeleweka baada ya kupokea ombi lako. Chombo husika kikikataa kubadilisha habari hizo kulingana na ombi lako, ni lazima kikujulishe juu ya katao hilo na kikushauri juu ya haki ya kusikilizwa kwa kusudi hili kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Nafasi ya Kusikilizwa. NAFASI YA KUSIKILIZWA 34 CFR §300.619 Chombo husika lazima, ikiombwa, kitoe nafasi ya kusikilizwa ili habari katika rekodi za elimu kuhusu mtoto wako zipingwe ili kuhakikisha kwamba ni sahihi, hazipotoshi, au kama sivyo hazikeuki siri au haki zingine za mtoto wako. UTARATIBU WA KUSIKILIZWA 34 CFR §300.621 Kusikilizwa ili kupinga habari ndani ya rekodi za elimu lazima zitekelezwa kulingana na utaratibu wa kusikilizwa chini ya Sheria ya Siri na Haki za Elimu ya Jamii (FERPA). MATOKEO YA KUSIKILIZWA 34 CFR §300.620 Ikiwa, kama matokea ya kusikilizwa, chombo husika kikiamua kwamba habari si sahihi, zinapotosha, au kama sivyo zinakeuka siri au haki zingine za mtoto, ni lazima kibadilishe habari hizo vilivyo na kikujulishe kwa kuandika. Ikiwa, kama matokeo ya kusikilizwa, chombo husika kikiamua kwamba habari hizi si sahihi, zinapotosha, au kama sivyo zinakeuka siri au haki za mtoto, ni lazima kikujulishe juu ya haki yako ya kuweka katika rekodi hizo ambazo kinatunza juu ya mtoto wako taarifa ikitoa maoni juu ya habari hizo au ikitoa sababu zozote za kukataa uamuzi wa chombo husika. Ufafanuzi kama huo unaowekwa katika rekodi za mtoto wako ni lazima: 1. Zitunzwe na chombo husika kama sehemu ya rekodi za mtoto wako maadamu rekodi hiyo au sehemu iliyokataliwa itunzwe na chombo husika; na 10 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 2. Chombo husika kikifichua rekodi za mtoto wako au sehemu iliyokataliwa kwa chama chochote, ufafanuzi lazima ufichuliwe kwa chama hicho pia. RUHUSA YA KUFICHUA HABARI ZA KIBINAFSI ZINAZOWEZA KUTAMBULIWA 34 CFR §300.622 Isipokuwa habari hizo ziwe katika rekodi za elimu, na ufichuzi umeidhinishwa bila ruhusa ya mzazi chini ya sheria ya Siri na Haki ya Elimu ya Jamii (FERPA), ruhusa yako lazima ipatikane kabla ya habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa kufichuliwa kwa vyama kando na maafisa wa vyombo husika. Isipokuwa chini ya hali zilizoelezwa hapo chini, ruhusa yako haitakikani kabla ya habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa kufichuliwa kwa maafisa wa vyombo husika kwa makusudi ya kufikia mahitaji ya Sehemu B ya IDEA. Ruhusa yako, au ruhusa ya mtoto anayestahiki ambaye amefikia umri wa wengi chini ya Sheria za Serikali, lazima ipatikane kabla ya habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa kufichuliwa kwa maafisa wa vyombo husika vinavyotoa au kulipia huduma za mabadiliko. Ikiwa mtoto wako yuko, au anaenda shule ya kibinafsi ambayo haipo katika wilaya ya shule moja unayoishi, ruhusa yako lazima ipatikane kabla ya habari yoyote ya kibinafsi inayoweza kutambuliwa kuhusu mtoto wako kufichuliwa kati ya maafisa katika wilaya shule ambapo shule hiyo ya kibinafsi ipo na maafisa katika wilaya ya shule ambapo wewe unaishi. KUHIFADHI 34 CFR §300.623 Kila chombo husika lazima kilinde siri ya habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa wakati wa kukusanywa, kutunzwa, kufichuliwa, na kuharibiwa. Afisa mmoja kwa kila chombo husika lazima achukue uwajibikaji wa kuhakikisha siri ya habari zozote za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa. Watu wote wanaokusanya au kutumia habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa lazima wapokee mafunzo au maagizo yanayohusiana na sera na utaratibu wa Serikali kuhusu siri chini ya Sehemu B ya IDEA na Sheria ya Siri na Haki ya Elimu ya Jamii (FERPA). Kila chombo husika lazima kidumishe orodha mpya ya majina na vyeo vya wafanyakazi walio katika chombo hicho ambao wanaweza kufikia habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa ili umma iweze kuchunguza. UHARIBIFU WA HABARI 34 CFR §300.624 Wilaya ya shule yako lazima ikujulishe wakati habari za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa ambazo zilikusanywa, zilitunzwa, au zilitumiwa hazihitajiki tena ili kutoa huduma za kielimu kwa mtoto wako. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Habari hizo lazima ziharibiwe wewe ukiomba. Walakini, rekodi ya kudumu ya jina la mtoto wako, anwani, na namba ya simu, gredi yake, rekodi ya kuhudhuria, darasa alizohudhuria, kiwango cha gredi aliyokamilisha, na mwaka aliyomaliza inaweza kutunzwa bila kizuizi cha wakati. 11 Utaratibu wa Malalamiko ya Serikali UTOFAUTI KATI YA MALALAMIKO YA KUSIKILIZWA KWA MCHAKATO UNAOTAZAMIWA NA UTARATIBU WA MALALAMIKO YA SERIKALI Maagizo ya Sehemu B ya IDEA imeweka utaratibu tofauti wa Malalamiko ya Serikali na malalamiko ya mchakato unaotazamiwa na kusikilizwa. Kama ilivyofafanuliwa hapo chini, mtu yeyote au shirika lolote linaweza kuwasilisha malalamiko ya Serikali kwa kudai ukeukaji wa mahitaji ya Sehemu yoyote ya B na wilaya ya shule, Chombo cha Elimu cha Serikali, au chombo chochote cha umma. Ni wewe tu au wilaya ya shule inaweza kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa juu ya suala lolote linalohusiana na pendekezo au kutoanzisha au kubadilisha kitambulisho, tathmini au mahali pa elimu ya mtoto mlemavu, au utoaji wa elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) kwa mtoto. Ijapokuwa Wafanyakazi wa Chombo cha Elimu cha Serikali kwa ujumla lazima watatue malalamiko ya Serikali kati ya muda maalum wa siku 60 za kalenda, isipokuwa muda huo maalum uongezwe vizuri, afisa wa kusikiliza mchakato adilifu unaotazamiwa lazima asikilize malalamiko ya mchakato unaotazamiwa (ikiwa haujatatuliwa kupitia mkutano wa suluhisho au kupitia mapatano) na apeane uamuzi ulioandikwa kati ya siku 45 za kalenda baada ya mwisho wa kipindi cha suluhisho, kama ilivyofafanuliwa kwenye hati hii chini ya kichwa cha Mchakato wa Suluhisho, isipokuwa afisa wa kusikiza aongeze muda maalum wewe ukiomba au wilaya ya shule ikiomba. Malalamiko ya Serikali na malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, utaratibu wa suluhisho na kusikilizwa yamefafanuliwa zaidi hapo chini. KUCHUKULIWA KWA UTARATIBU WA MALALAMIKO YA SERIKALI 34 CFR §300.151 Kwa ujumla Kila Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kiwe na utaratibu ulioandikwa wa: 1. Kutatua malalamiko yoyote, pamoja na malalamiko yaliyowasiishwa na shirika au mtu kutoka Jimbo lingine; 2. Kuwasilishwa kwa malalamiko na Chombo cha Elimu cha Serikali; 3. Kusambaza zaidi utaratibu wa malalamiko ya Serikali kwa wazazi na watu wengine wanaopendezwa, pamoja na vituo vya habari na vya kuwafunza wazazi, vyombo vya ulinzi na uwakili, vituo vya kuishi vyenye kujitegemea, na vitu vingine vinavyofaa. 12 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Marekebisho ya kunyimwa huduma muhimu Katika kutatua malalamiko ya Serikali ambayo Chombo cha Elimu cha Serikali kimepata ukosefu wa kutoa huduma muhimu, Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kishughulikie: 1. Ukosefu wa kutoa huduma muhimu, pamoja na hatua sahihi muhimu ya kushughulikia mahitaji ya mtoto; na 2. Utoaji muhimu wa usoni wa huduma kwa watoto wote walemavu. UTARATIBU WA CHINI WA MALALAMIKO YA SERIKALI 34 CFR §300.152 Kizuizi cha wakati; Utaratibu wa chini Kila Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kijumuishe katika utaratibu wake wa malalamiko ya serikali kizuizi cha wakati wa siku 60 za kalenda baada ya malalamiko kuwasilishwa ili: 1. Kitekeleze uchunguzi wenye kujitegemea wa mahali hapo, ikiwa Chombo cha Elimu cha Serikali kikiamua kwamba uchunguzi ni muhimu; 2. Kumpa mwenye kulalamika nafasi ya kuwasilisha habari zaidi, aidha kwa kusema au kwa kuandika, kuhusu madai kwenye malalamiko; 3. Kupatia wilaya ya shule au chombo kingine cha umma nafasi ya kujibu malalamiko, pamoja na; (a) kwa chaguo la chombo; pendekezo la kutatua malalamiko; na (b) nafasi ya mzazi kuwasilisha malalamiko na chombo kukubali kwa kujitolea kujihusisha katika mapatano: 4. Kuhakiki habari zote muhimu na kufanya uamuzi wa kibinafsi wa kama wilaya ya shule au chombo kingine cha umma kinakeuka mahitaji ya Sehemu B ya IDEA; na 5. Kupeana uamuzi ulioandikwa kwa mwenye kulalamika ambao unashughulikia madai kwenye malalamiko na inayojumuisha: (a)kweli na hitimisho iliyopatikana ; na (b) sababu za uamuzi wa mwisho wa Chombo cha Elimu cha Serikali. Muda kuongezwa; uamuzi wa mwisho; utekelezaji Utaratibu wa chombo cha Elimu cha Serikali uliofafanuliwa hapo juu lazima pia: 1. Iruhusu kuongezwa kwa kizuizi cha wakati wa siku 60 tu za kalenda ikiwa: (a) hali za kipekee ziliopo kulingana na malalamiko ya Serikali maalum; au (b) wazazi na wilaya ya shule au chombo kingine cha umma kinachohusika kwa kujitolea kikubali kuongeza muda wa kutatua suala hilo kupitia upatanisho au njia zingine za kutatua mzozo, ikiwa inapatikana katika Serikali. 2. Ijumuishe utaratibu wa utekelezaji kamili wa uamuzi wa mwisho wa Chombo cha Elimu cha Serikali, ikitakikana, pamoja na: (a) shughuli za usaidizi wa kiufundi; (b) majadiliano; na (c) hatua sahihi za kufikia masharti. Malalamiko ya serikali na kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa Malalamiko ya Serikali yaliyoandikwa yakipokewa ambayo pia ni suala la kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa kama ilivyofafanuliwa hapo chini chini ya kichwa cha Kuwasilisha Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa, au malalamiko ya Serikali yanajumuisha masuala kadhaa ambayo moja au zaidi ni sehemu ya kusikilizwa kama huko, Serikali lazima iweke kando malalamiko ya Serikali, au sehemu yoyote ya malalamiko ya Serikali ambayo yanashughulikiwa katika kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa hadi kusikilizwa huko kuishe. Suala lolote katika 13 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu malalamiko ya Serikali ambayo sio sehemu ya kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa lazima itatuliwe kwa kutumia kizuizi cha wakati na utaratibu uliofafanuliwa hapo juu. Suala likizuka katika malalamiko ya Serikali ambalo liliamuliwa hapo awali katika kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ikijumuisha vyama vile vile (wewe na wilaya ya shule), kisha uamuzi wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa uwe wa kubana kwa suala hilo na Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kimjulishe mwenye kulalamika kwamba uamuzi ni wa kubana. Malalamiko yanayodai wilaya ya shule au chombo kingine cha umma kilikosa kutekeleza uamuzi wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa lazima yatatuliwe na Chombo cha Elimu cha Serikali. KUWASILISHA MALALAMIKO 34 CFR §300.153 Shirika au mtu anaweza kuwasilisha Malalamiko ya Serikali yaliyoandikwa na kutiwa saini chini ya utaratibu uliofafanuliwa hapo juu. Malalamiko ya Serikali lazima yajumuishe: 1. Taarifa ya kwamba wilaya ya shule au chombo kingine cha umma kimekeuka hitaji la Sehemu B ya IDEA au maagizo yake; 2. Ukweli wa msingi wa taarifa hii; 3. Saini na habari ya anwani ya mwenye kulalamika; na 4. Ikiwa unadai ukeukaji kuhusu mtoto fulani: (a) Jina la mtoto na anwani ya makao ya mtoto huyo; (b) Jina la shule ambayo mtoto uhudhuria; (c) Katika hali ya mtoto au kijana asiye na makao, habari ya anwani ya mtoto huyo, na jina ya shule ambayo mtoto huyo anahudhuria; (d) Ufafanuzi wa hali ya shida ya mtoto, pamoja na kweli zinazohusiana na shida hiyo; na (e) Suluhisho iliyopendekezwa ya shida hiyo na vile inavyojulikana na kupatikana kwa chama kinachowasilisha malalamiko hayo wakati malalamiko yalipowasilishwa. Malalamiko hayo lazima yadai ukeukaji uliofanyika zaidi ya mwaka mmoja kabla ya tarehe ambayo malalamiko yalipokewa kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Kuchukuliwa kwa Utaratibu wa Malalamiko ya Serikali. Chama kinachowasilisha malalamiko lazima kipeleke mbele nakala ya malalamiko kwa wilaya ya shule au chombo kingine cha umma kinachohudumia mtoto huyo kwa wakati mmoja ambao chama hicho kinawasilisha malalamiko hayo kwa Chombo cha Elimu cha Serikali. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 14 Utaratibu wa Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa KUWASILISHA MALALAMIKO YA MCHAKATO UNAOTAZAMIWA 34 CFR §300.507 Kwa ujumla Wewe au wilaya ya shule inaweza kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa juu ya suala lolote linalohusiana na pendekezo au kutoanzisha au kubadilisha kitambulisho, tathmini au mahali pa elimu ya mtoto wako, au utoaji wa elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) kwa mtoto. Malalamiko ya mchakato unaotazamiwa lazima udai ukeukaji ambao ulitendeka baada ya miaka miwili kabla wewe au wilaya ya shule ilijua au ilipaswa kujua kuhusu hatua iliyodaiwa ambayo uunda msingi wa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. Muda maalum ulio hapo juu hautumiki ikiwa hauwezi kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa kati ya muda maalum kwa sababu: 1. Wilaya ya shule haswa ilitafsiri vibaya kwamba ilikuwa imetatua masuala yaliyotambuliwa kwenye malalamiko; au 2. Wilaya ya shule ilikuficha habari ambazo ilipaswa kukupa chini ya Sehemu B ya IDEA. Habari kwa wazazi Wilaya ya shule lazima ikujulishe kuhusu huduma zozote muhimu za bure za kisherea au za gharama ya chini zinazopatikana katika eneo ikiwa utaomba habari hizo, au wewe au wilaya ya shule ikiwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. MALALAMIKO YA MCHAKATO UNAOTAZAMIWA 34 CFR §300.508 Kwa ujumla Ndiposa kuomba kusikilizwa, wewe au wilaya ya shule (au wakili wako au wakili wa wilaya ya shule) lazima awasilishe malalamiko ya mchakato unaotazamiwa kwa chama kile kingine. Malalamiko hayo lazima yajumuishe yote yaliyomo yaliyoorodheshwa na lazima yawekwe siri. Wewe au wilaya ya shule, yoyote aliyewasilisha malalamiko hayo, lazima pia apatie Chombo cha Elimu cha Serikali nakala ya malalamiko. Yaliyomo kwenye malalamiko Malalamiko ya mchakato unaotazamiwa lazima yajumuishe: 1. Jina la mtoto; 2. Anwani ya makao ya mtoto; 3. Jina la shule ya mtoto; 4. Ikiwa mtoto ni mtoto au kijana ambaye hana makao, habari za mawasiliano ya mtoto na jina la shule ya mtoto; 15 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 5. Ufafanuzi wa hali ya shida ya mtoto inayohusiana na hatua iliyopendekezwa au kukataliwa, pamoja na kweli zinazohusiana na shida hiyo; na 6. Suluhisho iliyopendekezwa ya shida hiyo na vile inavyojulikana na kupatikana kwako au wilaya ya shule kwa wakati huo. Ilani inayohitajika kabla ya kusikilizwa kwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa Wewe au wilaya ya shule mwaweza kukosa kupata kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa hadi wewe au wilaya ya shule (au wakili wako au wakili wa wilaya ya shule), awakilishe malalamiko ya mchakato unaotazamiwa ambao unajumuisha habari zilizoorodheshwa hapo juu. Utoshelevu wa malalamiko Ndiposa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa yaendelee mbele, lazima yaonekane kwamba yanatosha. Malalamiko ya mchakato unaotazamiwa yataonekana yakutosha (yatakuwa yamefikia mahitaji ya yaliyomo hapo juu) isipokuwa chama kinachopokea malalamiko ya mchakato unaotazamiwa (wewe au wilaya ya shule) kimjulishe afisa wa kusikiliza na chama kile kingine kwa kuandika, kati ya siku 15 za kalenda baada ya kupokea malalamiko hayo, ya kwamba chama kinachopokea kinaamini kwamba malalamiko ya mchakato unaotazamiwa haufikii mahitaji yaliyoorodheshwa hapo juu. Kati ya siku tano za kalenda baada ya kupokea taarifa, chama kinachopokea (wewe au wilaya ya shule) kitaonelea malalamiko ya mchakato unaotazamiwa kuwa hayatoshi, afisa wa kusikiliza lazima amue kama malalamiko ya mchakato unaotazamiwa yanafikia mahitaji yaliyoorodheshwa hapo juu, na akuarifu wewe na wilaya ya shule kwa kukuandikia mara moja. Kurekebishwa kwa malalamiko Wewe au wilaya ya shule inaweza kufanya mabadiliko kwa malalamiko kama tu: 1. Chama kile kingine kikiidhinisha mabadiliko kwa kuandika na kimepewa nafasi ya kutatua malalamiko ya mchakato unaotazamiwa kupitia mkutano wa suluhisho, uliofafanuliwa hapo chini; au 2. Isipite siku tano kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa, afisa wa kusikiliza apeane ruhusa ya mabadiliko hayo. Ikiwa chama kinacholalamika (wewe au wilaya ya shule) kikifanya mabadiliko kwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, muda maalum wa mkutano wa suluhisho (kati ya siku 15 za kalenda baada ya kupokea malalamiko) na kipindi cha muda wa suluhisho (kati ya siku 30 za kalenda baada ya kupokea malalamiko) huanza tena siku ile malalamiko yaliyorekebishwa huwasilishwa. Majibu ya chombo cha elimu cha mtaani (LEA) au wilaya ya shule kwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. Ikiwa wilaya ya shule haijakutumia ilani iliyoandikwa mapema, kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Ilani Iliyoandikwa Mapema, kuhusu suala kuu katika malalamiko yako ya mchakato unaotazamiwa, wilaya ya shule lazima, kati ya siku 10 za kalenda baada ya kupokea malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, ikutumie majibu ambayo yanajumuisha: 1. Ufafanuzi wa kwanini wilaya ya shule ilipendekeza au ilikataa kuchukua hatua iliyoletwa katika malalamiko ya mchakato unaotazamiwa; 2. Ufafanuzi wa chaguzi zingine ambazo Kikundi cha mpango wa elimu ya kibinafsi ya mtoto wako (IEP) kilionelea na sababu ambazo chaguzi hizo zilikataliwa; 3. Ufafanuzi wa kila utaratibu wa tathmini, uchunguzi, rekodi au ripoti ambayo wilaya ya shule yako ilitumia kama msingi wa hatua iliyopendekezwa au kukataliwa; na 16 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 4. Ufafanuzi wa hali zingine ambazo ni muhimu kwa hatua iliyopendekezwa au kukataliwa ya wilaya ya shule. Kutoa habari kwenye vipengele 1-4 hapo juu haizuii wilaya ya shule kutokana na kusisitiza kwamba malalamiko yako ya mchakato unaotazamiwa haukutosha. Majibu ya chama kingine kwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa Isipokuwa kama ilivyosemwa chini ya kichwa-kidogo juu ya, Majibu ya chombo cha elimu cha mtaani (LEA) au wilaya ya shule kwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, chama kinachopokea malalamiko ya mchakato unaotazamiwa lazima, kati ya siku 10 za kalenda baada ya kupokea malalamiko, kitumie chama kile kingine majibu ambayo yanahutubia haswa masuala kwenye malalamiko hayo. FOMU ZA MFANO 34 CFR §300.509 Chombo cha Elimu cha Serikali kimeanzisha fomu za mfano ili kukusaidia wewe kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa na malalamiko ya Serikali. Walakini, haupaswi kutumia fomu hizi za mfano. Kwa kweli, unaweza kutumia mfano wa fomu hiii au fomu nyingine inayofaa, maadamu ina habari zinazohitajika za kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa au malalamiko ya Serikali. Ili upate fomu za mfano unaweza kufanya yanayofuata: 1. Pakua kutoka kwa tovuti hii – http://www.dese.mo.gov/divspeced/Complaint_System/index.htm 2. Pigia simu Idara ya Missouri ya Elimu ya Msingi na ya Upili, nambari ya simu (573) 751-0602. UPATANISHO 34 CFR §300.506 Kwa ujumla Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kifanye upatanisho upatikane ili wewe na wilaya ya shule iruhusiwe kutatua mizozo inayohusiana na suala lolote chini ya Sehemu B ya IDEA, pamoja na masuala yanayotokea baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. Hivyo basi, upatanisho unapatikana ili kutatua mizozo chini ya Sehemu B ya IDEA, iwe umewasilisha au haujawasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa ili kuomba kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Kuwasilisha Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa. Mahitaji Utaratibu lazima uhakikishe kwamba mchakato wa upatanisho: 1. Ni wa kujitolea kwa upande wako na kwa upande wa wilaya ya shule; 2. Haujatumiwa kukunyima au kuchelewesha haki yako ya kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa, au kukataa haki zingine zozote ambazo unazo chini ya Sehemu B ya IDEA; na 17 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 3. Umetekelezwa na mpatanishaji aliyehitimu na asiye na upendeleo ambaye amefunzwa kuhusu mbinu kamili za upatanisho. Ili kuomba upatanisho tuma ombi lililoandikwa kwa: Idara ya Missouri ya Elimu ya Msingi na ya Upili Divisheni ya Elimu Maalum/Sehemu ya Maafikiano PO Box 480 Jefferson City, MO 65102-0480 Wilaya ya shule inaweza kuanzisha utaratibu ambao unawapa wazazi na shule ambazo zinachagua kutotumia mchakato wa upatanisho, nafasi ya kupatana, kwa wakati na mahali panapofaa kwako, na chama ambacho ni cha haki: 1. Ambaye amebanwa na kandarasi na chombo kingine maalum cha kutatua mzozo, au kituo cha habari na cha kuwafunza wazazi au kituo cha habari cha wazazi wa jamii katika Serikali; na 2. Ambaye atafafanua manufaa na akuimize utumie mchakato wa upatanisho. Serikali lazima iwe na orodha ya watu ambao ni wapatanishaji waliohitimu na wanaojua sheria na masharti yanayohusiana na toleo la elimu maalum na huduma zinazolingana. Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kiwachague wapatanishaji kwa mpangilio usio na utaratibu, kwa kuzunguka, au njia zingine za haki. Serikali inauwajibikaji wa gharama ya mchakato wa upatanisho, pamoja na gharama za mikutano. Kila mkutano katika mchakato wa upatanisho lazima upangwe kwa njia ya muda na ufanywe mahali panapofaa kwako na wilaya ya shule. Wewe na wilaya ya shule mkitatua mzozo kupitia mchakato wa upatanisho, vyama vyote lazima viingie kwa makubaliano ya kisheria yanayobana ambayo yanaorodhesha suluhisho hilo na: 1. Inayosema kwamba majadiliano yote yaliyofanywa wakati wa mchakato wa upatanisho utabakia siri na hauwezi kutumiwa kama ushahidi katika kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa au kesi ya umma; na 2. Imetiwa saini na wewe na mwakilishi wa wilaya ya shule ambaye anaidhini ya kubana wilaya ya shule. Makubaliano yaliyoandikwa, na kutiwa saini yanaweza kulazimishwa katika korti yoyote ya Serikali yenye mamlaka ya kisheria (korti ambayo inamamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hii chini ya sheria za Serikali) au katika korti ya wilaya ya Marekani. Majadiliano ambayo yalifanyika wakati wa mchakato wa upatanisho lazima yawe siri. Hayawezi kutumiwa kama ushahidi katika kusikilizwa kwowote kwa usoni kwa mchakato unaotazamiwa au kesi ya umma ya korti yoyote ya Jimbo au korti ya Serikali ya Jimbo linalopokea usaidizi chini ya Sehemu B ya IDEA. Uadilifu wa mpatanishaji Mpatanishaji huyo: 1. Hawezi kuwa mfanyakazi wa Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule ambayo inahusika katika elimu au ulezi wa mtoto wako; na 2. Lazima asiwe na upendeleo wa kibinafsi au wa kikazi ambao unazozana na madhumuni ya mpatanishaji. 18 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Mtu ambaye anahitimu kama mpatanishaji si mfanyakazi wa wilaya ya shule au chombo cha Serikali kwa sababu yeye analipwa na chombo au wilaya ya shule ili ahudumu kama mpatanishaji. MAHALI PA MTOTO WAKATI KUSIKILIZWA NA MALALAMIKO YA MCHAKATO YAKISUBIRI 34 CFR §300.518 Isipokuwa kama ilivyotolewa hapo chini chini ya kichwa cha UTARATIBU UNAPOKUWA UKIWAFUNDISHA NIDHAMU WATOTO WALEMAVU, mara tu malalamiko ya mchakato unaotazamiwa unapotumwa kwa chama kile kingine, wakati wa kipindi cha muda wa mchakato wa suluhisho, na unaposubiri uamuzi wa kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa au kesi yoyote ya korti, isipokuwa wewe na Serikali au wilaya ya shule mkubaliane, mtoto wako lazima abakie mahali pake pa elimu alipo sasa. Ikiwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa yanahusisha maombi ya kuchukuliwa mara ya kwanza katika shule ya umma, mtoto wako, akiwa na ruhusu yako, lazima awekwe katika mpango wa kawaida wa shule ya umma hadi kukamilika kwa kesi hizo zote. Ikiwa malalamiko ya mchakato unaotazamiwa yanahusisha maombi ya huduma ya kwanza chini ya Sehemu B ya IDEA ya mtoto ambaye anabadilika kutoka kwa huduma chini ya Sehemu C ya IDEA hadi Sehemu B ya IDEA na ambaye astahiki tena huduma za Sehemu C kwa sababu mtoto amefikia miaka mitatu, wilaya ya shule haipaswi kutoa huduma za Sehemu C ambazo mtoto huyo amekuwa akipokea. Mtoto huyo akipatikana anastahiki chini ya Sehemu B ya IDEA na umetoa ruhusa mtoto huyo apokee elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mara ya kwanza, basi, ukisubiri matokeo ya kesi, wilaya ya shule lazima itoe elimu maalum na huduma hizo zinazolingana ambazo hazina mizozo (zile ambazo wewe na wilaya ya shule mnakubaliana). MCHAKATO WA SULUHISHO 34 CFR §300.510 Mkutano wa suluhisho Kati ya siku 15 za kalenda baada ya kupokea ilani yako ya malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, na kabla ya kuanza kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa, wilaya ya shule lazima iite mkutano kati yako na wanachama wanaofaa wa Kikundi cha mpango wa elimu ya kibinafsi (IEP) ambao wanaufahamu maalum wa kweli zilizotambuliwa katika malalamiko yako ya mchakato unaotazamiwa. Mkutano huo: 1. Lazima uwe na mwakilishi wa wilaya ya shule ambaye anamlaka ya kufanya uamuzi kwa niaba ya wilaya ya shule; na 2. Hauwezi kuwa na wakili wa wilaya ya shule isipokuwa wewe umezindikishwa na wakili. Wewe na wilaya ya shule muamue wanachama wanaofaa wa Kikundi cha IEP watakaohudhuria mkutano huo. 19 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Madhumuni ya mkutano huo ni wewe ujadili malalamiko yako ya mchakato unaotazamiwa, na kweli ambazo zinaunda msingi wa malalamiko hayo, ili wilaya ya shule iwe na nafasi ya kutatua mzozo huo. Mkutano huo wa suluhisho sio lazima ikiwa: 1. Wewe na wilaya ya shule mkikubaliana kwa kuandika kuondoa mkutano huo; au 2. Wewe na wilaya ya shule mkikubaliana kutumia njia ya upatanisho, kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Upatanisho. Kipindi cha suluhisho Ikiwa wilaya ya shule haijatatua malalamiko ya mchakato unaotazamiwa hadi ukaridhika kati ya siku 30 za kalenda baada ya kupokea malalamiko ya mchakato unaotazamiwa (wakati wa kipindi cha muda wa mchakato wa suluhisho) kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa unaweza kufanywa. Muda maalum wa siku 45 za kalenda wa kutoa uamuzi wa mwisho huanza baada ya kuisha kwa siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho, na ruhusa zingine za marekebisho yaliyofanywa kwa siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho, kama ilivyofafanulia hapo chini. Isipokuwa mahali ambapo wewe na wilaya ya shule mmekubaliana kuondoa mchakato wa suluhisho au kutumia upatanisho, kukosa kwako kuhusika katika mkutano wa suluhisho kunaweza kuchelewesha muda maalum wa mchakato wa suluhisho na kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa hadi ukubali kuhusika katika mkutano. Ikiwa baada ya kufanya jitihada na kuandika jitihada hizo, wilaya ya shule haiwezi kukupata katika mkutano wa suluhisho, wilaya ya shule inaweza, wakati wa mwisho wa siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho, kuomba kwamba afisa wa kusikiliza atupilie mbali malalamiko yako ya mchakato unaotazamiwa. Kuandikwa kwa jitihada kama hizo lazima kujumuishe rekodi ya majaribo ya wilaya ya shule kupanga wakati na mahali mnapokubaliana wote, kama vile: 1. Rekodi za kina za simu zilizopigwa au zilizojaribiwa kupigwa na matokeo ya simu hizo; 2. Nakala za mawasiliano ulizotumiwa na majibu yoyote yaliyopokewa; na 3. Rekodi za kina za ziara zilizofanywa kwa nyumba yako au mahali pa ajira na matokeo ya ziara hizo. Wilaya ya shule ikikosa kufanya mkutano wa suluhisho kati ya siku 15 za kalenda baada ya kupokea ilani yako ya malalamiko ya mchakato unaotazamiwa au ikose kuhusika kwenye mkutano wa suluhisho, unaweza kumuuliza afisa wa kusikiliza atoe amri ya kwamba muda maalum wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamia huanze. Marekebisho ya siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho Wewe na wilaya ya shule mkikubali kwa kuandika kuondoa mkutano wa suluhisho, basi muda maalum wa siku 45 za kalenda za kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa huanza siku inayofuata. Baada ya kuanza kwa upatanisho au mkutano wa suluhisho na kabla ya mwisho wa siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho, wewe na wilaya ya shule mkikubali kwa kuandika kwamba hakuna makubaliano yanayowezekana, basi muda maalum wa siku 45 za kalenda za kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa huanza siku inayofuata. Wewe na wilaya ya shule mkikubali kutumia mchakato wa upatanisho, wakati wa mwisho wa siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho, vyama vyote vinaweza kukubali kwa kuandika kuendelea na upatanisho hadi makubaliano yapatikane. Walakini, wewe au wilaya ya shule 20 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu mkijiondoa kutoka kwa mchakato wa upatanisho, basi muda maalum wa siku 45 za kalenda wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa huanza siku inayofuata. Makubaliano yaliyoandikwa ya mahali Suluhisho la mzozo likifikiwa katika mkutano wa suluhisho, wewe na wilaya ya shule lazima muingie katika makubaliano ya kisheria yanayobana ambayo: 1. Yametiwa saini na wewe na mwakilishi wa wilaya ya shule ambaye anaidhini ya kubana wilaya ya shule; na 2. Yanaweza kulazimishwa katika korti yoyote ya Serikali yenye mamlaka ya kisheria (korti ambayo inamamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hiyo) au katika korti ya wilaya ya Marekani au na Chombo cha Elimu cha Serikali, ikiwa Jimbo lako halina mbinu nyingine au utaratibu mwingine ambao unaruhusu vyama kutafuta kulazimishwa kwa makubaliano ya suluhisho. Kipindi cha kuhakiki makubaliano Wewe na wilaya ya shule mkiingia katika makubaliano kama matokeo ya mkutano wa suluhisho, nyinyi wote (wewe au wilaya ya shule) mnaweza kubatilisha makubaliano hayo kati ya siku 3 za biashara baa ya wakati wewe na wilaya ya shule mlitia saini makubaliano hayo. Kusikilizwa kwa Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa KUSIKILIZWA KWA MCHAKATO ADILIFU UNAOTAZAMIWA 34 CFR §300.511 Kwa ujumla Wakati wowote malalamiko ya mchakato unaotazamiwa yanapowasilishwa, wewe au wilaya ya shule inayohusika katika mzozo huu lazima mpate nafasi ya kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa, kama ilivyofafanuliwa katika sehemu za Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa na Mchakato wa Suluhisho. Ombi lililoandikwa la kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa lazima litumwe kwa Idara ya Missouri ya Elimu ya Msingi na ya Upili, na lazima nakala itolewe na itumwe kwa chombo ambacho unaanzisha mchakato unaotazamiwa dhidi yake. Anwani ya kutuma barua ya Idara hiyo ni: MODESE Attention: Compliance Section/Special Education PO Box 480 21 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Jefferson City, MO 65102 Faksi: (573) 526-4404 Afisa mwadilifu wa kusikiliza Kwa uchache, afisa wa kusikiliza: 1. Lazima asiwe mfanyakazi wa Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule ambayo inahusika katika elimu au ulezi wa mtoto huyo. Walakini, mtu si mfanyakazi wa chombo kwa sababu yeye analipwa na chombo hicho ili kuhudumu kama afisa wa kusikiliza; 2. Lazima asiwe na upendeleo wa kibinafsi au wa kikazi ambao unazozana na madhumuni ya afisa wa kusikiliza wakati wa kusikilizwa. 3. Lazima awe anafahamu na kuelewa toleo za IDEA, na maagizo ya Jimbo na Serikali kuhusu IDEA, na ukalimani wa kisheria wa IDEA na korti za Jimbo na Serikali; na 4. Lazima awe na ufahamu na uwezo wa kutekeleza kusikilizwa, na kufanya na kuandika maamuzi, yanayoambatana na zoezi linalofaa la kawaida la kisheria. Kila wilaya ya shule lazima iweke orodha ya watu wale ambao wanahudumu kama maafisa wa kusikiliza ambayo inajumuisha taarifa ya sifa zinazostahili za kila afisa wa kusikiliza. Suala kuu la kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa Upande ambao unaomba kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa (wewe au wilaya ya shule) hauwezi kuleta masuala wakati wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ambao haukushughulikiwa katika malalamiko ya mchakato unaotazamiwa, isipokuwa upande ule mwingine ukubali. Muda maalum wa kuomba kusikilizwa Wewe au wilaya ya shule lazima iombe kusikilizwa adilifu juu ya malalamiko ya mchakato unaotazamiwa kati ya miaka miwili ya tarehe wewe au wilaya ya shule ilipojua au ilipaswa kujua kuhusu suala lililoshughulikiwa kwenye malalamiko. Kinzano za muda maalum Muda maalum ulio hapo juu hautumiki ikiwa haukuweza kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa kwa sababu: 1. Wilaya ya shule haswa ilitafsiri vibaya kwamba ilikuwa imetatua shida au suala ambalo unaleta katika malalamiko yako; au 2. Wilaya ya shule ilikuficha habari ambazo ilipaswa kukupa chini ya Sehemu B ya IDEA. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu HAKI ZA KUSIKILIZWA 22 34 CFR §300.512 Kwa ujumla Upande wowote wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa (pamoja na kusikilizwa kunakohusiana na utaratibu wa kufunza nidhamu) una haki ya: 1. Kuzindikishwa na kushauriwa na wakili au watu walio na ufahamu maalum au mafunzo kuhusu shida za watoto walemavu; 2. Ushahidi wa sasa na kukabili, kuchunguza, na kuhitaji washahidi wahudhurie; 3. Kukataa kuletwa kwa ushahidi wowote wakati wa kusikilizwa ambao haujafichuliwa kwa chama hicho kabla ya siku tano za biashara kabla ya kusikilizwa; 4. Kupata rekodi iliyoandikwa ya kusikilizwa ya neno baada ya neno, au, kwa chaguo lako, ya elektroniki, na 5. Kupata matokeo ya kweli na maamuzi yaliyoandikwa, au, kwa chaguo lako, ya elektroniki. Ufichuaji zaidi wa habari Kwa uchache siku tano za biashara kabla ya kusikilizwa kwa mchakato unaotaziwa, wewe na wilaya ya shule lazima mfichue kwa yule mwingine tathmini zote zilizokamilika kabla ya tarehe hiyo na mapendekezo ambayo msingi wake ni tathmini hiyo ambayo wewe au wilaya ya shule mnakusudia kutumia wakati wa kusikilizwa. Afisa wa kusikiliza anaweza kuzuia chama chochote ambacho kinashindwa kufuata hitaji hili kutokana na tathmini inayofaa au mapendekezo wakati wa kusikilizwa bila ruhusa ya chama kile kingine. Haki za mzazi wakati wa kusikilizwa Lazima upewe haki ya: 1. Mtoto wako kuwepo; 2. Kufungua kusikilizwa kwa umma; na 3. Kupewa rekodi ya kusikilizwa, matokeo ya kweli na maamuzi bila gharama yoyote. MAAMUZI YA KUSIKILIZWA 34 CFR §300.513 Uamuzi wa afisa wa kusikiliza Uamuzi wa afisa wa kusikiliza wa kama mtoto wako alipokea elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) lazima msingi wake uwe misingi ya kweli. Katika hoja zinazodai ukeukaji wa utaratibu, afisa wa kusikiliza anaweza kupata kwamba mtoto wako hakupokea FAPE kama tu kupungukiwa kwa utaratibu: 1. Kuliingiliana na haki ya mtoto wako ya elimu ya bure inayofaa umma (FAPE); 2. Kuliingiliana vilivyo na nafasi yako ya kuhusika katika mchakato wa kufanya uamuzi kuhusu utoaji wa elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) kwa mtoto wako; au 3. Kulisababisha kupungukiwa kwa manufaa ya kielimu. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 23 Ibara ya uundaji Hamna toleo lolote lililofafanuliwa hapo juu linaweza kutafsiriwa kama kumzuia afisa wa kusikiliza kuamuru wilaya ya shule kufuata mahitaji kwenye sehemu ya kuhifadhi utaratibu ya maagizo ya Jimbo chini ya Sehemu B ya IDEA (34 CFR §§300.500 hadi 300.536). Ombi la kando la kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa Hakuna chochote kwenye sehemu ya kuhifadhi utaratibu wa maagizo ya Jimbo chini ya Sehemu B ya IDEA (34 CFR §§300.500 hadi 300.536) inaweza kutafsiriwa kama inakuzuia wewe kuwasilisha malalamiko ya kando ya mchakato unaotazamiwa juu ya suala kando na malalamiko ya mchakato unaotazamiwa ambao tayari umewasilishwa. Matokeo na uamuzi wa jopo la ushauri na umma kwa ujumla Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule, (yeyote aliyewajibika kwa kusikilizwa kwako) baada ya kufuta habari zozote za kibinafsi zinazoweza kutambuliwa, lazima: 1. Atoe matokeo na maamuzi ya kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa au akate rufaa kwa jobo la ushauri wa elimu maalum ya Serikali; na 2. Afanye matokeo hayo na maamuzi hayo yapatikane kwa umma. Kukata rufaa KUKAMILIKA KWA UAMUZI; KUKATA RUFAA; UHAKIKI ADILIFU 34 CFR §300.514 Kukamilika kwa uamuzi wa kusikilizwa Uamuzi unaofanywa wakati wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa (pamoja na kusikilizwa kunakohusiana na utaratibu wa kufunza nidhamu) ni wa mwisho, isipokuwa kama chama chochote kinachohusika katika kusikilizwa (wewe au wilaya ya shule) kikate rufaa juu ya uamuzi huo kwa kuleta hatua ya madai, kama ilivyofafanuliwa hapo chini. MUDA MAALUM NA URAHISI WA KUSIKILIZWA NA UHAKIKI 34 CFR §300.515 Chombo cha Elimu cha Serikali lazima kihakishe kwamba isipite siku 45 za kalenda baada ya kuisha kwa siku 30 za kalenda za kipindi cha mkutano wa suluhisho au, kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa-kidogo cha Marekebisho ya siku 30 za kalenda za kipindi cha suluhisho, isipite siku 45 za kalenda baada ya kuisha kwa kipindi cha muda uliorekebishwa: 1. Uamuzi wa mwisho ufikiwe kwa kusikilizwa, na 2. Nakala ya uamuzi itumwe kwa kila chama. Afisa wa kusikiliza anaweza kuongeza muda maalum zaidi ya kipindi cha muda wa siku 45 za kalenda hapo juu chama chochote kikiomba. 24 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Kila kusikilizwa lazima kufanywe kwa wakati na mahali ambapo ni rahisi kwako na kwa mtoto wako. HATUA ZA MADAI, PAMOJA NA KIPINDI CHA MUDA AMBAO UNAWEZA KUWASILISHA HATUA HIZO 34 CFR §300.516 Kwa ujumla Chama chochote (wewe au wilaya ya shule) kisichokubali matokeo na uamuzi wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa (pamoja na kusikilizwa kunakohusiana na utaratibu wa kufunza nidhamu) kinahaki ya kuleta hatua ya madai inayohusiana na hoja ambayo ilikuwa suala la kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa. Hatua hiyo inaweza kuletwa kwa korti ya Serikali yenye mamlaka ya kisheria (korti ya Serikali ambayo inamamlaka ya kusikiliza kesi ya aina hii) au katika korti ya wilaya ya Merikani bila kuzingatia ukubwa wa mzozo. Kizuizi cha muda Chama ambacho kinaleta hatua hiyo (wewe au wilaya ya shule) kitakuwa na siku 45 za kalenda kuanzia tarehe ya uamuzi wa afisa wa kusikiliza wa kuwasilisha hatua ya madai. Utaratibu zaidi Katika hatua yoyote ya madai, korti: 1. Hupokea rekodi za msimamizi wa kesi; 2. Husikia ushahidi zaidi wewe ukiomba au wilaya ya shule ikiomba; na 3. Huweka uamuzi wake kwa kuwepo kwa ushahidi na hupeana msaada ambao korti huonelea unafaa. Mamlaka ya kisheria ya korti za wilaya Korti za wilaya za Marekani zina mamlaka ya kutoa uamuzi wa hatua zilizoletwa chini ya Sehemu B ya IDEA bila kuzingatia ukubwa wa mzozo. Sheria ya uundaji Hakuna kitu chochote katika Sehemu B ya IDEA kinachopinga au kuzuia haki, utaratibu na marekebisho yanayopatikana chini ya Katiba ya Marekani, Sheria ya 1990 ya Waamerika walemavu, Kichwa cha V cha sheria ya Urekebishaji ya 1973 (Sehemu ya 504), au sheria zingine za Jimbo zinazolinda haki za watoto walemavu, isipokuwa kama kabla ya kuwasilishwa kwa hatua ya madai chini ya sheria hizi ukitafuta msaada ambao unapatikana pia chini ya Sehemu B ya IDEA, utaratibu wa mchakato unaotazamiwa uliofafanuliwa hapo juu lazima utumiwe kabisa kama vile ingelivyotumiwa kama inavyohitajika ikiwa chama hicho kingewasilisha hatua hiyo chini ya Sehemu B ya IDEA. Hii inamaanisha kwamba unaweza kuwa na marekebisho yanayopatikana chini ya sheria zingine ambazo zinapitana na zile zinazopatikana chini ya IDEA, ili upate usaidizi chini ya sheria hizo, lakini kwa ujumla, lazima kwanza utumie marekebisho ya msimamizi yanayopatikana chini ya IDEA (k.v., malalamiko ya 25 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu mchakato unaotazamiwa, mkutano wa suluhisho, na utaratibu wa kusikilizwa kwa mchakato adilifu unaotazamiwa) kabla ya kwenda moja kwa moja kortini. ADA YA WAKILI 34 CFR §300.517 Kwa ujumla Katika hatua yoyote au kesi iliyoletwa chini ya Sehemu B ya IDEA, ukiendelea, korti, kwa kupendelea kwake, inaweza kutuza ada ya wakili kama sehemu ya gharama kwako. Katika hatua yoyote au kesi iliyoletwa chini ya Sehemu B ya IDEA, korti, kwa kupendelea kwake, inaweza kutuza ada ya wakili kama sehemu ya gharama kwa Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule, ilipwe na wakili wako, ikiwa wakili huyo: (a) amewasilisha malalamiko au kesi ya korti ambayo korti inapata ni hafifu, isiyoeleweka, au isio na msingi ; au (b) ameendelea kuenda mahakamani baada ya madai kuwa hafifu, yasiyoeleweka, au yasio na msingi; au Katika hatua yoyote au kesi iliyoletwa chini ya Sehemu B ya Idea, korti, kwa kupendelea kwake, inaweza kutuza ada ya wakili kama sehemu ya gharama kwa Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule, ilipwe na wakili wako, ikiwa ombi lako la kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa au kesi ya baadaye ya korti ililetwa kwa sababu zisizostahili, kama vile kunyanyasa, kusababisha upotezaji wa wakati, au kuongeza gharama ya hatua hiyo au kesi hiyo. Tuzo la ada Korti hutuza ada ya wakili kama inavyofuata: 1. Ada lazima msingi wake iwe viwango vilivyo kwenye jamii ambayo hatua hiyo au kusikilizwa kulianza kwa aina na uzuri wa huduma zilizotolewa. Hakuna bonasi au kichanganyiko kinachoweza kutumiwa katika kuhesabu ada itakayotuzwa. 2. Ada haiwezi kutuzwa na gharama zinazolingana haziwezi kurudishwa katika hatua au kesi yoyote chini ya Sehemu B ya IDEA ya huduma zilizotekelezwa baada ya toleo uliloandikiwa la maafikiano ikiwa: a. Toleo hilo limefanywa kati ya muda uliofafanuliwa na Sheria ya 68 ya Sheria za Jimbo za Utaratibu wa Madai au, katika hali ya kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa au uhakiki wa kiwango cha Serikali, wakati wowote zaidi ya siku 10 za kalenda kabla ya kesi kuanza; b. Toleo hilo halikubaliwi kati ya siku 10 za kalenda; na c. Korti au afisa msimamizi wa kusikiliza akipata kwamba usaidizi ambao ulipata mwishowe haukufai zaidi ya toleo lile lingine la maafikiano. Licha ya vizuizi hivi, tuzo la ada ya wakili na gharama zinazohusiana zinaweza kufanywa kwako ikiwa utaendelea na kama ulihesabiwa haki kwa kukataa toleo la maafikiano. 3. Ada inayohusiana na mkutano wowote wa Kikundi cha elimu ya kibinafsi (IEP) haitatuzwa isipokuwa mkutano huo ufanywe kama matokeo ya msimamizi wa kesi au hatua ya korti. Mkutano wa suluhisho, kama ilivyofanuliwa chini ya kichwa cha Mkutano wa suluhisho, hauchukuliwi kama mkutano ulioitwa kama matokeo ya kusikilizwa kwa msimamizi au Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 26 hatua ya korti, na pia haichukuliwi kama kusikilizwa kwa msimamizi au hatua ya korti kwa madhumuni ya toleo hizi za ada ya wakili. Korti hupunguza, kama inavyostahili, kiwango cha ada ya wakili inayotuzwa chini ya Sehemu B ya IDEA, kama korti itapata kwamba: 1. Wewe, au wakili wako, wakati wa mkondo wa hatua au kesi, mlichelewesha suluhisho la mwisho la mzozo; 2. Kiwango cha ada ya wakili kiilichoidhinishwa kituzwe kilipita kiwango cha kila saa kiliopo katika jamii kwa huduma sawa ya mawakili wenye ustadi, sifa na ujuzi huo mmoja. 3. Muda uliochukuliwa na huduma za kisheria zilizotolewa zilipita kiasi kulingana na hali ya hatua au kesi; au 4. Wakili anayekuwakilisha hakupatia wilaya ya shule habari zinazofaa katika ilani ya ombi la mchakato unaotazamiwa kama ilivyofafanuliwa chini ya kichwa cha Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa. Walakini, korti haiwezi kupunguza ada ikiwa korti itapata kwamba Serikali au wilaya ya shule ilichelewesha suluhisho la mwisho la hatua au kesi au kulikuwa na ukeukaji chini ya utoaji wa kuhifadhi utaratibu ya Sehemu B ya IDEA. Utaratibu unapokuwa ukiwafundisha nidhamu watoto walemavu MAMLAKA YA MTUMISHI WA SHULE 34 CFR §300.530 Uamuzi wa kesi kwa kesi Mtumishi wa shule anaweza kuzingatia hali yoyote ya kipekee kwa misingi ya kesi kwa kesi, wakati unapoamua kubadilisha mahali, iliyofanywa kulingana na mahitaji yanayofuata yanayohusiana na tabia, inamfaa mtoto mlemavu ambaye anakeuka kanuni ya shule ya mwenendo wa mwanafunzi. Kwa ujumla Kwa kadiri kwamba pia wanachukua hatua kama hiyo kwa watoto wasio na ulemavu, mtumishi wa shule anaweza, kwa siku zisizopita 10 za shule zikifuatana, kumwondoa mtoto mlemavu ambaye anakeuka kanuni za mienendo ya wanafunzi kutoka mahali pake pa sasa hadi kwa mpangilio mwingine wa elimu ya muda unaofaa (ambayo lazima iamuliwe na Kikundi cha mpango wa elimu ya kibinafsi (IEP)), mpangilio mwingine, au kusimamishwa. Mtumishi wa shule pia anaweza kuongeza uhamisho zaidi kwa mtoto kwa siku zisizopita 10 za shule zikifuatana katika mwaka huo mmoja wa shule kwa matukio tofauti za makosa, maadamu uhamisho huo haujumuishi mabadiliko ya mahali (angalia hapo chini Mabadiliko ya Mahali kwa sababu ya Uhamisho wa Kinidhamu kwa ajili ya ufafanuzi). Mara tu mtoto mlemavu akihamishwa kutoka kwa mahali pake pa sasa kwa jumla ya siku 10 za shule katika mwaka mmoja wa shule, wilaya ya shule lazima, wakati wa siku za uhamisho zinazofuata katika mwaka huo wa shule, itoe huduma kama inavyotakikana hapo chini, chini ya kichwa-kidogo cha Huduma. 27 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Mamlaka ya ziada Ikiwa tabia iliyokeuka kanuni za mienendo ya wanafunzi haikuwa onyesho la ulemavu wa mtoto (angalia hapo chini Uamuzi wa onyesho) na mabadiliko ya kinidhamu ya mahali inaweza kupita siku 10 za shule zikifuatana, mtumishi wa shule anaweza kutumia utaratibu wa nidhamu kwa mtoto huyo mlemavu kwa njia sawa na muda sawa kama ingelivyokuwa kwa watoto wasio na ulemavu, isipokuwa shule hiyo lazima itoe huduma kwa mtoto huyo kama ilivyofafanuliwa hapo chini, chini ya Huduma. Kikundi cha mtoto cha EIP huamua mpangilio mwingine wa elimu ya muda kwa huduma kama hiyo. Huduma Huduma ambazo lazima zitolewe kwa mtoto mlemavu ambaye amehamishwa kutoka mahali pake pa sasa zinaweza kutolewa katika mpangilio mwingine wa elimu ya muda. Wilaya ya shule inahitajika tu kutoa huduma kwa mtoto mlemavu ambaye amehamishwa kutoka mahali pake pa sasa kwa siku 10 za shule au chini katika mwaka huo wa shule, ikiwa hutoa huduma kwa mtoto asiye na ulemavu ambaye amehamishwa vivyo hivyo. Mtoto mlemavu ambaye amehamishwa kutoka mahali pake pa sasa kwa zaidi ya siku 10 za shule lazima: 1. Aendelee kupokea huduma za kielimu, ili kumwezesha mtoto aendelee kuhusika katika mtalaa wa elimu ya jumla, ijapokuwa katika mpangilio mwingine, na kuendelea kuwadia kufikia malengo yaliyowekwa katika IEP ya mtoto; na 2. Apokee, kama inavyotakikana, uchunguzi unaotumika wa kitabia, na huduma za uingiliaji tabia na urekebishaji, ambazo zimeundwa ili kushughulikia ukeukaji wa tabia ili isifanyike tena. Baada ya mtoto mlemavu kuhamishwa kutoka mahali pake pa sasa kwa siku 10 za shule katika mwaka huo mmoja wa shule, na ikiwa uhamisho wa sasa ni wa siku 10 za shule zikifuatana au chini na ikiwa uhamisho huo sio mabadiliko ya mahali (angalia ufafanuzi hapo chini), basi mtumishi wa shule, kwa kushauriana na mmoja wa waalimu wa mtoto, anaweza kuamua umbali ambao huduma zitahitajika ili kumwezesha mtoto kuendelea kuhusika katika mtalaa wa elimu ya jumla, ijapokuwa katika mpangilio mwingine, na kuendelea kuwadia kufikia malengo yaliyowekwa katika IEP ya mtoto. Ikiwa uhamisho ni mabadaliko ya mahali (angalia ufafanuzi hapo chini), Kikundi cha mtoto cha IEP kitaamua huduma zinazofaaa ili kumwezesha mtoto kuendelea kuhusika katika mtalaa wa elimu ya jumla, ijapokuwa katika mpangilio mwingine, na kuendelea kuwadia kufikia malengo yaliyowekwa katika IEP ya mtoto. Uamuzi wa onyesho Kati ya siku 10 za shule za uamuzi wowote wa kubadilisha mahali pa mtoto mlemavu kwa sababu ya ukeukaji wa kanuni za mienendo ya wanafunzi (isipokuwa uhamisho ambao ni wa siku 10 za shule zikifuatana au chini na wala sio mabadiliko ya mahali), wilaya ya shule, mzazi, na wanachama wanaofaa wa Kikundi cha IEP (kama ilivyoamuliwa na mzazi na wilaya ya shule) lazima ahakiki habari zote zinazofaa katika faili ya mwanafunzi, pamoja na IEP ya mtoto, uchunguzi wowote wa mwalimu, na habari zozote zinazofaa zilizotolewa na wazazi ili waamue: 1. Kama mwenendo unaoshughulikiwa ulisababishwa, au ulikuwa na uhusiano dhabiti na wa moja kwa na ulemavu wa mtoto; au 2. Kama mwenendo unaoshughulikiwa ulikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya wilaya ya shule kukosa kutekeleza IEP ya mtoto. 28 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Ikiwa wilaya ya shule, mzazi, na wanachama wanaofaa wa Kikundi cha mtoto cha IEP wakiamua kwamba hali hizo zote zilifikiwa, mwenendo huo lazima uamuliwe kuwa ni onyesho la ulemavu wa mtoto. Ikiwa wilaya shule, mzazi, na wanachama wanaofaa wa Kikundi cha mtoto cha IEP wakiamua kwamba mwenendo unaoshughulikiwa ulikuwa matokeo ya moja kwa moja ya shule kukosa kutekeleza IEP, wilaya ya shule lazima ichukue hatua ya moja kwa moja ya kurekebisha upungufu huo. Uamuzi wa kwamba tabia ilikuwa onyesho la ulemavu wa mtoto Ikiwa wilaya ya shule, mzazi, na wanachama wanaofaa wa Kikundi cha IEP wakiamua kwamba mwenendo huo ulikuwa onyesho la ulemavu wa mtoto, Kikundi cha IEP aidha lazima: 1. Kifanye uchunguzi unaotumika wa kitabia, isipokuwa wilaya ya shule ilikuwa imefanya uchunguzo unaotumika wa kitabia kabla ya tabia ambayo ilisababisha mabadiliko yaliyofanywa ya mahali, na kutekeleza mpango wa kuingilia tabia ya mtoto; au 2. Ikiwa mpango wa uingiliaji wa kitabia tayari umeanzishwa, kihakiki mpango wa kuingilia tabia, na kuirekebisha kama inavyotakikana, ili ishughulikie tabia hiyo. Isipokuwa kama ilivyofafanuliwa hapo chini, chini ya kichwa-kidogo cha Hali maalum, wilaya ya shule lazima imrudishe mtoto huyo mahali ambapo mtoto huyo alihamishwa, isipokuwa wazazi na wilaya ikubali kubadilisha mahali hapo kama sehemu ya kurekebisha mpango wa kuingilia tabia. Hali maalum Iwe tabia ilikuwa onyesho la ulemavu wa mtoto au hapana, mtumishi wa shule anaweza kumwamisha mwanafunzi hadi kwa mpangilio mwingine wa elimu ya muda (inayoamuliwa na Kikundi cha mtoto cha IEP) hadi siku 45 za shule, ikiwa mtoto: 1. Anabeba silaha shuleni au ana silaha shuleni (angalia ufafanuzi hapo chini), kwa majengo ya shule, au kwa hafla ya shule chini ya mamlaka ya kisheria ya Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule; 2. Kwa kujua anatumia au ana madawa yasio halali (angalia ufafanuzi hapo chini), au anauza au anaomba mauzo ya kitu kinachodhibitiwa, (angalia ufafanuzi hapo chini), akiwa shuleni, kwa majengo ya shule, au kwa hafla ya shule chini ya mamlaka ya kisheria ya Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule; au 3. Amemuumiza mtu mwingine vibaya sana kimwili (angalia ufafanuzi hapo chini), akiwa shuleni, kwa majengo ya shule, au kwa hafla ya shule chini ya mamlaka ya kisheria ya Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule. Ufafanuzi Kitu kinachodhibitiwa inamaanisha dawa au kitu kingine kinachotambuliwa chini ya ratiba I, II, III, IV, au V katika sehemu ya 202 (c) ya Sheria ya Vitu Vinavyodhibitiwa (21 U.S.C. 812 (c)). Dawa isiyo halali inamaanisha kitu kinachodhibitiwa; lakini haijumuishi kitu kinachodhibitiwa ambacho kinamilikiwa kihalali au kutumiwa chini ya usimamizi wa mtaalam wa kimatibatu aliyeidhinishwa au ambayo inamilikiwa kihalali au kutumiwa chini ya utawala mwingine chini ya Sheria hiyo au chini ya utoaji mwingine wowote wa Sheria ya Serikali. Kuumizwa vibaya sana kimwili ina umaana uliyopewa neno la "kuumizwa vibaya sana kimwili" chini ya aya ya (3) ya sehemu ndogo ya (h) ya sehemu ya 1365 ya kichwa cha 18, Kanuni za Marekani. 29 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu Silaha ina umaana uliyopewa neno la “silaha hatari” chini ya aya ya (2) ya sehemu ndogo ya kwanza ya (g) ya sehemu ya 930 ya kichwa cha 18, Kanuni za Marekani. Taarifa Tarehe ile ambayo uamuzi unafanywa wa kufanya uhamisho ambao ni mabadiliko ya sehemu ya mtoto kwa sababu ya ukeukaji wa kanuni za mienendo ya wanafunzi, wilaya ya shule lazima iwajulishe wazazi juu ya uamuzi huo, na iwapatie wazazi ilani ya kuhifadhi utaratibu. MABADILIKO YA MAHALI KWA SABABU YA UHAMISHO WA KINIDHAMU 34 CFR §300.536 Kuhamishwa kwa mtoto mlemavu kutoka mahali pake pa sasa pa elimu ni mabadiliko ya mahali ikiwa: 1. Uhamisho huo ni wa zaidi ya siku 10 za shule zikifuatana; au 2. Mtoto huyo amepitia misururu ya uhamisho ambayo yanajumuisha mtindo kwa sababu: a. Misururu hiyo ya uhamisho kwa ujumla ni zaidi ya siku 10 za shule kwa mwaka wa shule; b. Tabia ya mtoto ni sawa kabisa na tabia ya mtoto huyo katika matukio ya hapo awali ambayo yalisababisha misururu hiyo ya uhamisho; c. Kama vile mambo ya ziada kama urefu wa kila uhamisho, ujumla wa kiwango cha wakati ambao mtoto huyo amehamishwa, na kukaribiana kwa uhamisho na ule mwingine; na Iwe au isiwe mtindo wa uhamisho unaojumuisha mabadiliko ya mahali yanaamuliwa kwa misingi ya kesi kwa kesi na wilaya ya shule na, kama itapingwa, inaweza kuhakikiwa kupitia mchakato unaotazamiwa na kesi ya kisheria. UAMUZI WA MPANGILIO 34 CFR §300.531 Kikundi cha mpango wa kibinafsi wa elimu (IEP) lazima kiamue mpangilio mwingine wa elimu ya muda ya uhamisho ambayo ni mabadiliko ya mahali, na uhamisho chini ya kichwa cha Mamlaka ya ziada na Hali maalum, hapo juu. Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu KUKATA RUFAA 30 34 CFR §300.532 Kwa ujumla Mzazi wa mtoto mlemavu anaweza kukata rufaa ya malalamiko ya mchakato unaotazamiwa (angalia hapo juu) ili aombe kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ikiwa yeye hakubaliani na: 1. Uamuzi wowote unaohusiana na mahali uliofanywa chini ya utoaji wa tabia; au 2. uamuzi wa onyesho uliofafanuliwa hapo juu. Wilaya ya shule inaweza kuwasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa (angalia hapo juu) ili aombe kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ikiwa anaamini kwamba kutunza mahali pa sasa pa mtoto kunaweza kusababisha kuumia kwa mtoto au kuumia kwa wengine. Mamlaka ya afisa wa kusikiliza Afisa wa kusikiliza ambaye anafikia mahitaji yaliyofafanuliwa chini ya kichwa-kidogo cha Afisa mwadilifu wa kusikiliza lazima atekeleze kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa na afanye uamuzi. Afisa wa kisikiliza anaweza: 1. Kumrudisha mtoto mlemavu mahali ambapo mtoto huyo alihamishwa ikiwa afisa wa kusikiliza ataamua kwamba uhamisho huo ulikuwa ukeukaji wa mahitaji yaliyofafanuliwa chini ya kichwa cha Mamlaka ya mtumishi wa shule, au kwamba tabia ya mtoto ilikuwa onyesho la ulemavu wa mtoto; au 2. Kuamuru mabadiliko ya mahali pa mtoto mlemavu hadi kwa mpangilio mwingine wa elimu ya muda isiyozidi siku 45 za shule ikiwa afisa wa kusikiliza akiamua kwamba kutunza mahali pa sasa pa mtoto inaweza kusababisha kuumia kwa mtoto au kuumia kwa wengine. Utaratibu huu wa kusikilizwa unaweza kurudiwa, ikiwa wilaya ya shule inaamini kwamba kumrudisha mtoto mahali pake pa asili inaweza kusababisa kuumia kwa mtoto au kuumia kwa wengine. Wakati wowote mzazi au wilaya ya shule inapowasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa ya kuomba kusikilizwa kama huko, kusikilizwa lazima kufanyike ambako kunafikia mahitaji yaliyofafanuliwa chini ya vichwa vya Utaratibu wa Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa, Kusikilizwa kwa Malalamiko ya Mchakato Unaotazamiwa, isipokuwa kama ifwatavyo: 1. Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule lazima ifanye mipango ya kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ulioharakishwa, ambao lazima ufanywe kati ya siku 20 za shule kwanzia tarehe ya maombi ya kusikilizwa na lazima itoe matokeo ya uamuzi kati ya siku 10 za shule baada ya kusikilizwa. 2. Isipokuwa wazazi na wilaya ya shule ikubali kuondoa mkutano kwa kuandika, au ikubali kutumia upatanisho, mkutano wa suluhisho lazima ufanyike kati ya siku saba za kalenda baada ya kupokea ilani ya malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. Kusikilizwa kunaweza kuendelea isipokuwa suala hilo liwe limetatuliwa hadi vyama vyote viridhike kati ya siku 15 za kalenda baada ya kupokea malalamiko ya mchakato unaotazamiwa. 3. Serikali inaweza kuanzisha sheria tofauti za utaratibu ili kuharakisha kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa zaidi ya vile ilivyoanzisha kwa kusikilizwa kwingine kwa mchakato unaotazamiwa, lakini isipokuwa kwa muda maalum, sheria zile ambazo 31 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu lazima zifuatane na sheria ndani ya hati hii kuhusiana na kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa. Chama kinaweza kukata rufaa uamuzi wa kusikilizwa kwa mchakato unaotazamiwa ulioharakishwa kwa njia sawa na kama vile kiwezavyo kwa kusikilizwa kwingine kwa mchakato unaotazamiwa (angalia Kukata rufaa, hapo juu). MAHALI WAKATI WA KUKATA RUFAA 34 CFR §300.533 Kama ilivyofafanuliwa hapo juu, wakati wazazi au wilaya ya shule inapowasilisha malalamiko ya mchakato unaotazamiwa unaohusiana na masuala ya kinidhamu, mtoto lazima abakie kwa mpangilio mwingine wa elimu ya muda akisubiri uamuzi wa afisa wa kusikiliza, au hadi kuisha kwa kipindi cha muda wa kuhamishwa kama ilivyotolewa na kufafanuliwa chini ya kichwa cha Mamlaka ya Mtumishi wa Shule, yoyote itakayofanyika kwanza (isipokuwa mzazi na Chombo cha Elimu cha Serikali au wilaya ya shule ikubali) ULINZI KWA WATOTO AMBAO HAWAJASTAHIKI ELIMU MAALUM NA HUDUMA ZINAZOLINGANA 34 CFR §300.534 Kwa ujumla Ikiwa mtoto hajaamuliwa kwamba anastahiki elimu maalum na huduma zinazolingana na akeuke kanuzi za mienendo ya wanafunzi, lakini wilaya ya shule iwe ilijua (kama ilivyoamuliwa hapo chini) kabla ya tabia hiyo ambayo ilisababisha hatua iliyofanyika ya kinidhamu, ya kwamba mtoto huyo alikuwa mtoto mlemavu, basi mtoto huyo anaweza kudai ulinzi wowote uliofafanuliwa katika ilani hii. Misingi ya ufahamu kwa masuala ya kinidhamu Wilaya ya shule lazima ionekane kuwa ilijua kwamba mtoto ni mtoto mlemavu ikiwa, kabla ya tabia ambayo ilisababisha hatua iliyofanyika ya kinidhamu: 1. Mzazi wa mtoto huyo alionyesha shaka kwa kuandika kwamba mtoto huyo anahitaji elimu maalum na huduma zinazolingana kwa mtumishi mwangalizi au msimamizi wa chombo kinachofaa cha elimu, au mwalimu wa mtoto huyo; 2. Mzazi aliomba tathmini inayohusiana na kustahiki elimu maalum na huduma zinazolingana chini ya Sehemu B ya IDEA; au 3. Mwalimu wa mtoto huyo, au mtumishi mwingine wa wilaya ya shule alionyesha shaka maalum kuhusu mtindo wa kitabia ulionyeshwa na mtoto huyo moja kwa moja kwa mkurugenzi wa wilaya ya shule ya elimu maalum au kwa mtumishi mwingine mwangalizi wa wilaya ya shule. Kinzano Wilaya ya shule haitaonekana kuwa ilijua ikiwa: 1. Mzazi wa mtoto hakuruhusu tathmini ya mtoto au alikataa huduma ya elimu maalum; au 32 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 2. Mtoto ametathminiwa na akaamuliwa kuwa si mtoto mlemavu chini ya Sehemu B ya IDEA. Hali zinazotumika kama hakuna misingi ya ufahamu Ikiwa kabla ya kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtoto, wilaya ya shule haikuwa ikijua kwamba mtoto ni mtoto mlemavu, kama ilivyofafanuliwa hapo juu chini ya kichwa-kidogo cha Misingi ya ufahamu kwa masuala ya kinidhamu na Kinzano, mtoto huyo anaweza kupitia hatua za kinidhamu ambazo zinatumika kwa watoto wasio walemavu ambao hujihusisha na tabia kama hizo. Walakini, kama ombi litafanywa la tathmini ya mtoto wakati wa kipindi cha muda ambao mtoto anapitia hatua za kinidhamu, tathmini hiyo lazima itekelezwe kwa njia ya upesi. Hadi tathmini hiyo ikamilike, mtoto hubakia katika mahali pa elimu palipoamuliwa na utawala wa shule, ambayo inaweza kujumuisha kusimamishwa au kufukuzwa bila huduma za kielimu. Ikiwa mtoto ataamuliwa kuwa mtoto mlemavu, tukizingatia habari kutoka kwa tathmini iliyofanywa na wilaya ya shule, na habari zilizotolewa na wazazi, wilaya ya shule lazima itoe elimu maalum na huduma zinazolingana kulingana na Sehemu B ya IDEA, pamoja na mahitaji ya kinidhamu yaliyofafanuliwa hapo juu. REJELEO LA HATUA YA WATEKELEZA SHERIA NA WATAWALA WA KIMAHAKAMA 34 CFR §300.535 Sehemu B ya IDEA: 1. Haizuilii chombo kutokana na kuripoti uhalifu uliofanywa na mtoto mlemavu kwa utawala unaofaa; au 2. Haiwazuilii watekelezaji sheria wa Serikali na watawala wa kimahakama kutokana na kutekeleza uwajibikaji wao kuhusu kutumiwa kwa Sheria ya Jimbo na Serikali juu ya uhalifu uliofanywa na mtoto mlemavu. Upitishaji wa rekodi Wilaya ya shule ikiripoti uhalifu uliofanywa na mtoto mlemavu, wilaya ya shule: 1. Lazima ihakikishe kwamba nakala za rekodi za kinidhamu na elimu maalum ya mtoto zimepitishwa ili zizingatiwe na utawala ambao chombo hicho kiliripoti uhalifu huo; na 2. Inaweza kupitisha nakala za rekodi za kinidhamu na elimu maalum ya mtoto kwa kadiri iliyoidhinishwa na Sheria ya Siri na Haki ya Elimu ya Jamii (FERPA). Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu 33 Mahitaji ya Mahali pamoja ya Wazazi wa Watoto walio katika Shule za Kibinafsi kwa Gharama ya Umma KWA UJUMLA 34 CFR §300.148 Sehemu B ya IDEA haihitaji wilaya ya shule ilipie gharama ya elimu, pamoja na elimu maalum na huduma zinazolingana, za mtoto wako mlemavu aliye katika shule ya kibinafsi au jengo ikiwa wilaya ya shule ilifanya elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) ipatikane kwa mtoto wako na wewe ukachagua kumweka mtoto wako katika shule ya kibinafsi au jengo. Walakini, wilaya ya shule ambayo shule ya kibinafsi ipo lazima imjumuishe mtoto wako kati ya watu ambao mahitaji yao yameshughulikiwa chini ya utoaji wa Sehemu B kuhusu watoto ambao wamewekwa na wazazi wao katika shule ya kibinafsi chini ya 34 CFR §§300.131 hadi 300.144. Kurudishiwa gharama ya kuwekwa katika shule ya kibinafsi Ikiwa mtoto wako hapo awali alipokea elimu maalum na huduma zinazolingana chini ya utawala wa wilaya ya shule, na uchague kumwandikisha mtoto wako katika shule ya mapema ya kibinafsi, shule ya msingi, au shule ya upili bila ruhusa au kuelekezwa na wilaya ya shule, korti au afisa wa kusikiliza anaweza kuhitaji chombo hicho kikurudishie gharama ya kuandikishwa huko ikiwa korti au afisa wa kusikiliza atapata kwamba chombo hicho hakikufanya elimu ya bure inayofaa umma (FAPE) ipatikane kwa mtoto wako kwa wakati unaofaa kabla ya kuandikishwa huko na kwamba mahali hapo pa kibinafsi panafaa. Afisa wa kusikiliza au korti inaweza kupata kwamba mahali hapo panafaa, hata kama mahali hapo hapafikii viwango vya Serikali ambavyo vinatumika kwa elimu iliyotolewa na Chombo cha Elimu cha Serikali na wilaya ya shule. Kizuizi cha kurudishiwa gharama Gharama itakayorudishwa iliyofafanuliwa katika aya iliyo hapo juu inaweza kupunguzwa au kukataliwa: 1. Ikiwa: (a) Katika mkutano wa hivi karibuni wa mpango wa elimu ya kibinafsi (IEP) ambayo ulihudhuria kabla ya mtoto wako kuhamishwa kutoka kwa shule ya umma, haukujulisha kikundi cha IEP kwamba ulikuwa ukikataa mahali ambapo palipendekezwa na wilaya ya shule ili itoe FAPE kwa mtoto wako, pamoja na kusema hoja yako na lengo lako la kumwandikisha mtoto wako katika shule ya kibinafsi kwa gharama ya umma; au (b) Kabla ya siku 10 za biashara kabla ya mtoto wako kuhamishwa kutoka kwa shule ya umma (pamoja na siku zozote za mapumziko ambazo zinatokea wakati wa siku za biashara), haukupeana ilani iliyoandikwa kwa wilaya ya shule juu ya habari hizo; 2. Ikiwa, kabla ya mtoto wako kuhamishwa kutoka kwa shule ya umma, wilaya ya shule ilikupa ilani iliyoandikwa mapema, juu ya lengo lake la kumtathmini mtoto wako (pamoja na taarifa ya madhumuni ya tathmini ambayo ilifaa na iliyokuwa ya busara), lakini haukufanya mtoto apatikane kwa ajili ya tathmini hiyo; au 3. Baada ya matokeo ya korti ya kuwa hatua zako hazikuwa za busara. Walakini, gharama itakayorudishwa: 1. Lazima isipunguzwe wala kunyimwa kwa kukosa kutoa ilani ikiwa: (a) Shule ilikuzuia usitoe ilani hiyo; (b) Haukupokea ilani ya uwajibikaji wako wa kutoa ilani hiyo 34 Sehe mu B Ilani ya Kuhifadhi Utaratibu iliyofafanuliwa hapo juu; au (c) Kufuata mahitaji yaliyo hapo juu yangesababisha madhara ya kimwili kwa mtoto wako; na 2. Korti ikipendelea au afisa wa kusikiliza akipendelea, haitapunguzwa au kunyimwa kwa ajili ya wazazi kukosa kutoa ilani iliyohitaji ikiwa: (a) Mzazi hajasoma au hawezi kuandika Kiingereza; au (b) Kufuata mahitaji yaliyo hapo juu yanaweza kusababisha madhara makali ya kihisia kwa mtoto. Habari zaidi kuhusu kuhifadhi utaratibu wako inaweza kupatikana kutoka kwa ifuatayo: Idara ya Missouri ya Elimu ya Msingi na ya Upili Sehemu ya Maafikiano Simu: 573-751-0699 Faksi: 573-526-5946 TDD: 1-800-735-2966 Hatua ya Wazazi wa Missouri (MPACT) Simu: 816-531-7070 Faksi: 816-531-4777 TDD/Sauti: 1-800-743-7634 Octoba 2006 Idara ya Missouri ya Elimu ya Msingi na ya Upili Idara ya Elimu ya Msingi na ya Upili katika mipango yake na shughuli zake Haibagui kwa misingi ya umbari, rangi, asili ya kitaifa, jinsia, ulemavu, au umri. Maswali yanayohusiana na mipango ya Idara yanaweza kuelekezwa kwa Jefferson State Office Building, Title IX Coordinator, 5th Floor, 205 Jefferson Street, Jefferson City, MO 65102-0480; nambari ya simu 573-751-4212.